* Awataka wanasiasa kuacha kubeza imani za watu
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MATUMIZI mabaya ya mitandao ya kijamii yameelezwa kuzorotesha bunifu zenye tija katika jamii badala yake watu wamejikita katika kueneza, kusambaza, na kujaribu kuthibitisha taarifa za uongo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Makonda amesema kuwa upotoshaji katika mitandao ya kijamii umezidi kushamiri na kuwataka wakazi wa jiji hilo na wanajamii kwa ujumla kujihadhari na maneno wasiyoyafahamu na yasiyo na ukweli.
"Mtu akisema akisema uongo mara moja akabainika atengwe katika jamii, kueneza habari za uongo katika mitandao ya kijamii ambayo inatumiwa na idadi kubwa ya watu ni kuendelea kuathiri watu kwa kuwafanya kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kibunifu zenye tija badala yake wanapambana na masuala ya uongo kwa kujaribu kutafuta ukweli" ameeleza Makonda.
Kuhusiana na kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ya kuwataka wananchi kushiriki shughuli za kimaendeleo na kuabudu kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili sio kushinda kwenye nyumba za ibada kila siku Makonda ametengua kauli hiyo na kusema kuwa, Serikali haina dini na amewataka wananchi kuendelea na ibada bila kuathiri shughuli za kiserikali.
Amesema kuwa wanasiasa wawe makini wanapoongea kuhusiana na dini;
" Tuwe na kiasi tunapoongelea imani za watu, Mungu anaabudiwa kila siku wana Ilala endeleeni kuabudu na si vyema kupanga siku za kuabudu" amesema Makonda.
RC Paul Makonda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...