Picha ya kwanza vijana watakaoshiriki kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mratibu wa kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro kupeleka malengo ya endelevu ya maendelevu ya UN ,Munyaradzi Muzenda kutoka nchini Zimbambwe.

Vijana kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamejipanga kupanda Mlima Kilimanjaro lengo likiwa ni kuhamasisha vijana kushiriki katika kutimiza Malengo endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo watakuwa wa kwanza kupeleka bango la malengo hayo katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Munyaradzi Muzenda ni Mratibu wa Mpango huo kutoka nchini Zimbambwe anasema kuwa wanaendesha kampeni ya Mlima Kilimanjaro ishi ndoto zako ambayo inalenga kuhasisha malengo endelevu ya UN pamoja na kuhamasisha malengo Umoja wa Afrika 263 ya Afrika tunayoitaka.

Munyaradzi alisema kuwa jumla ya vijana 17 watapanda na vibao vya malengo hayo wakijikita zaidi kwenye lengo namba moja la Kupondoa Umasikini na kuhimiza vijana kushiriki katika shughuli zitakazosaidia kutokomeza umasikini.

Aidha amesema kuwa Tanzania itakua nchi ya kwanza duniani kupeleka malengo hayo katika mlima huo wa pili kwa urefu duniani hivyo amewataka wadau kuungana katika kampeni hiyo ya kupanda mlima mwishoni mwaka huu.

“Vijana kutoka mataifa mbalimbali watafika Arusha kwa ajili ya kupanda mlima na tunatarajia kampeni hiyo itafanikiwa kwa kiasi kikubwa” Alisema Munyaradzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...