Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za SADC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye hifadhi ya Taifa Arusha(ANAPA)wakiongozana na Ujumbe kutoka Tanzania
Wataalamu kutoka sekta za Utalii na Mazingira na Maliasili walioshiriki mkutano huo wa SADC wakiwa katika Hifadhi ya Taifa Arusha (ANAPA )
wajumbe wa mkutano wakitazama wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA)
Na Vero Ignatus,Arusha
Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za SADC wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA) wakiongozana na ujumbe wa Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo makundi ya wanyamapori kama vile nyati, nyumbu, pundamilia pamoja na maporomoko ya maji.
Ziara hiyo imelenga kuhamasisha utalii katika nchi wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania ambayo ina vivutio vingi vya utalii ambavyo ni mbuga za wanyama, hifadhi pamoja na utalii wa utamaduni.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Agnes Kayole ameeleza kufurahishwa na hifadhi ya Taifa ya Arusha ambayo ipo karibu na Mjini na ina vivutio vingi ikiwemo wanyama na maporomoko ya maji jambo ambalo linahitaji kutangazwa ili kupata watalii wengi zaidi.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Kitengo cha Utalii kutoka Wizara ya Utalii nchini Msumbiji Bw. Nosto Mazivile amefurahishwa na vivutio hivyo vizuri na kusisitiza kuwa vikitangazwa vizuri vitasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kutoa rai kwa Tanzania kuendelea na juhudi za kutunza na kuhifadhi kwa maendeleo endelevu.
Mhifadhi wa Masuala ya Utalii na Masoko kutoka Afrika Kusini , Rollen Fovak amesema kuwa ni mara ya kwanza kutembelea hifadhi hiyo ambapo wamejionea Ngurudoto Kreta, nyani weupe maarufu kama mbega pamoja na mapromoko ya maji ya Tululusia hivyo anajukumu la kuhamasisha mataifa mengine kutembelea hifadhi.
Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii zinandelea na vikao vyake kwa nchi wanachama wa SADC ambavyo vimeanza tarehe 21/10/2019 na vinatarajiwa kukamilika siku ya Ijumaa tarehe 25/10/2019 Jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...