Mratibu wa Mawasiliano Taifa wa Chama cha ACT, Mbarala Maharagande (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa Program za jamii taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Mwanaharusi Bunduki na kushoto ni Naibu katibu Mkuu Ngome ya  vijana Taifa ACT-Wazalendo, Boniphancia Mapunda.

Leandra Gabriel na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
CHAMA cha ACT Wazalendo kimemshauri Waziri wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Sulemani Jafo kutatua changamoto mbalimbali ndani ya siku zilizobaki kabla ya kuelekea uchaguuzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.

Akizungumza leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mawasiliano Taifa wa Chama cha ACT, Mbarala Maharagande amesema kuwa Waziri Sulemani Jafo anapaswa kutambua kuwa kuna njama ovu na hujuma dhidi ya vyama vya upinzani kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa unaoelekea kufanyika.

"Kuna tofauti kati ya hujuma au njama ovu na dosari au mapungufu, hujuma na njama ovu hizi zinafanywa dhidi ya vyama vya upinzani na wagombea wake pekee na hakuna lalamiko hata moja tulilolisikia au kushuhudia kutoka kwa CCM nchi nzima. Hii maana yake ni kwamba huenda hujuma hizo zinaratibiwa na Ofisi yake na wala hazitokei kwa bahati mbaya,"amesema Maharagande.

Amesema kuwa dosari zilizopo ofisi zinazosimamia uchakuguzi huo ikiwa ni kutokuwa na mihiri, kufungwa kwa ofisi, wagombea kutokupewa nakala za fomu za kugombea katika vijiji, kata na vitongoji. Ametaja maeneo yenye dosari hizo ambazo ni Ruangwa, Liwale, Bukombe, Songwe, Tabora, Busanda, Misungwi, Moshi Mjini, Morogoro Kusini Mashariki, Kasulu Vijijini, Tanga, Dar es Salaam, Newala, Mkoa wa Pwani na Mbeya.

"Tangu mchakato wa uchukuaji wa fomu uanze tarehe Oktoba 29, 2019 wanachama 276,401 wamejitokeza nchini kote kugombea nafasi za uongozi kupitia ACT-Wazalendo huku idadi hiyo ikiongezeka siku hadi siku na miongoni mwao kufanikiwa kuchukua fomu za kugombea".  Amesema Maharagande.

Pia Maharagande amesema Waziri Jafo achukue hatua dhidi ya viongozi watakaokiuka kanuni, taratibu, sheria na miongozo ya usimamizi wa uchaguzi.Hata hivyo amewaasa viongozi wa dini na wastaafu kuhimiza kutenda kwa Haki na kukemea viashiria vya kupotea kwa amani na utulivu kwani amani ni tunda la haki na pia kuamrisha kutenda mema kuendelea kukataza maovu.

Kwa upande wake Katibu wa Programu za Jamii Taifa wa ACT Mwanaharusi Bunduki amewashauri wasimamizi wa uchaguzi kupitia Serikali kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya kusimamia uchaguzi hiyo ili kuendelea kuitunza amani ya nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...