Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .
Jeshi la Polisi limesema kuwa mtu aliyemtishia hadharani kwa bunduki mwenzake anatafutwa kutokana na kosa la kutumia silaha kinyume na sheria ya umiliki wa silaha .
Kauli hiyo imetokana na kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtu mmoja akimtishia mwenzake katika mazingira ambayo hayakuwa na sababu ya mmiliki wa bunduki kutumia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema kuwa watu wamemilikishwa silaha sio kwa ajili ya kutishia watu wengine.
Sirro amesema kuwa mtu huyo aliyemtishia anatafutwa, na silaha hiyo inatakiwa kunyang'anywa kutokana na kuitumia vibaya.
Aidha amesema kuwa wananchi wanaopewa silaha wanapaswa kuacha kutumia vibaya, kwani wanaomba kwa sababu maalum matokeo yake wanatumia silaha visivyo.
"Watu wanatumia silaha visivyo,sasa Jeshi la polisi linamtafuta na popote akikamatwa sheria itashika mkondo wake kwa kutumia silaha vibaya kwa kutishia wananchi"amesema Sirro.
Sirro amesema kuwa silaha hizo zimekuwa zikiombwa kwa sababu ambazo wanaamini ni kwa matumiza sahihi na salama,lakini kwa makosa yanayopatikana kwa baadhi ya watu wanaokiuka taratibu za matumizi ya silaha hiyo/hizo hatua lazima zichukuliwe.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...