Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza mara baada ya kumaliza mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika nchini Ivory Cost.
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeongeza mtaji wa Benki hiyo kutoka dola za kimarekani bilioni 90 hadi dola za kimarekani 283 kutokana na uwepo wa majadiliano juu ya kiwango cha ongezeko la mtaji wa Benki.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, uliofanyika Abidjan Nchini Ivory Coast na kuhudhuriwa na Rais wa nchi ya Ivory Coast, Alassane Ouattara, amesema kuwa enki ya maendeleo ya Kilimo imeongeza mtaji wake kwa lengo la kukuza kilimo.

Prof. Kabudi amesema kuwa maamuzi yaliyopitishwa na magavana wa benki hiyo waliohudhuria mkutano huo ni ya kihistoria ambapo sasa inaifanya Benki ya Maendeleo ya Afrika kushika nafasi ya pili duniani baada ya Benki ya Dunia.

Amesema kuwa uamuzi huo unaifanya Benki ya Maendeleo Afrika kuwa na uwezo mkubwa wa kufadhili na kuhisani miradi mbalimbali na mikubwa ya kimkakati katika Bara la Afrika Tanzania ikiwemo na hivyo kuliwezesha bara hilo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Prof. Kabudi amezitaja faida ambazo nchi za Afrika itazipata kutokana na kuongezeka kwa mtaji wa Benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa mikopo mikubwa na ufadhili kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ajili ya kuliendeleza bara hilo husani katika miundo mbinu, nishati na hudumu muhimu za kijamii ambayo nchi nyingi za kiafrika ambazo ni wanachama wa benki hiyo walishindwa kuitekeleza kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila kwa upande wake amesema kutokana na Bara la Afrika kuwa na Nchi nyingi masikini uwepo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika inatoa ahueni kwa Nchi hizo na kutoa wito pia kwa taasisi binafsi kutoka nchi za Kiafrika kuchangamkia fursa ya ongezeko la mtaji wa Benki hiyo kutokana na ukweli kuwa AfDB inakopesha pia taasisi binafsi.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo ilianzishwa kwa lengo la kuchochea maendeleo ya Bara hilo ikiwa na jukumu la kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya kiuchumi ya Afrika inamilikiwa kwa asilimia 60 na nchi za kiafrika na asilimia nyingine 40 zilizosalia zinamilikiwa na nchi waalikwa kutoka katika mabara mengine duniani Marekani ikiwemo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...