Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza na Wanahabari leo katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar,kuhusu kufunguliwa kwa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao unatarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Balozi wa Swedeni nchini Tanzania Bi.Elisabeth Jacobsen akifafanua jambo mbele ya Wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja K. Mnyepe.Picha na Michuzi JR (MMG).
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Anders Sjoberg akizungumza na Wanahabari katika mkutano uliofanyika leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki wa Nchi tano za Nordic katika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 unaotarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. pichani kati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe na kushoto ni Balozi wa Swedeni nchini Tanzania Bi.Elisabeth Jacobsen
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza na Wanahabari leo katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar leo,kuhusu kufunguliwa kwa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao unatarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Anders Sjoberg akifafanua jambo kwa Wanahabari katika mkutano uliofanyika leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki wa Nchi tano za Nordic kushiriki katika mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 unaotarajiwa kuanza kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Picha na Michuzi JR (MMG).
Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu
RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kufungua mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao utaanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania.
Katika mkutano huo unatarajiwa kuwa na wageni zaidi ya 250 huku Watanzania wakishauriwa kuendeleza utamaduni wao kwa kuwakaribisha wageni wote watakaoshiriki na kwamba watumie fursa zitokanazo na uwepo wa mkutano huo kwa kufanya shughuli halali zitakazowanufaisha kiuchumi.
Akizungumza kuhusu mkutano huo leo Novemba 1,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam Katibu Mjuu Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Faraja Mnyepe amesema kwa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na masuala ya amani na usalama.
Amefafanua mkutano huo utajadili fursa za Uwekezaji, biashara,amani na usalama na masuala mengine mtambuka kama vile athari za mabadiliko ya tabianchi .Pia mawaziri hao watazungumza kuhusu uhusiano baina ya nchi yetu na nchi moja moja na hasa ubia wa kimaendeleo.
"Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano ,wenzetu wa Afrika na Nordoc watapenda pia kusikia uzoefu wa mafanikio ya Tanzania kwenye sekta za afya, elimu, nishati, miundombinu, kilimo ,utalii ,ukusanyaji wa kodi , mafanikio ya vuta dhidi ya rushwa, ujangili ,dawa za kulevya na maeneo mengine,"amesema Dk.Mnyepe.
Akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo amesema utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNICC) jijini Dar es Salaam na utafunguliwa na Rais Magufuli.
Amesema mkutano huo utajumuisha jumla ya mawaziri 34 wa mambo ya nje wa nchi za Afrika na Nordic pamoja na washiriki wengine ambao idadi yao inatarajiwa kufika milioni 250.Mawaziri ambao watakuja kutoka nchi za Nordic ni wa nchi za Sweden, Norway, Denmark, Finland, na Iceland.
Wakati nchi za kutoka Afrika ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso Burundi, Comoros, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) Misri, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho ,Mali, Malawi, Morocco, Msumbiji , Namibia, Nigeria, Niger, Rwanda, Senegal, Somalia, Afrika Kusini, ,Tunisia, Uganda, Zambia, Zimbwabwe, na Tanzania ambayo ndio mwenyeji.
Dk.Mnyepe amesema mkutano huo utajumuisha mawaziri, mabalozi, wa nchi shiriki za Afrika katika nchi za Nordic ,mabalozi wa nchi za Nordic pamoja na watendaji wa Serikali .Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu inasema " Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu".
Ameeleza ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Nordic ni wa kihistoria na wa pekee na kwamba ushirikiano huo ulianza hata kabla ya Uhuru wa Tanganyika ambapo Wamisionari kutoka nchi hizo walikuja kufanya kazi hapa nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu.
Pia amesema ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa vinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika,urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika.
Dk.Mnyepe amesema katika nchi za Afrika ,Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi za Nordic kuliko nchi nyingine yoyote.Kwa mfano kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2013 mpaka 2018 Tanzania imepokea takribani Sh.bilioni 900 kutoka nchi za Nordic na kwamba nchi hizo zimekuwa zikisaidia sekta mbalimbali.
Pia amesema wazo la kuanzishwa mkutano huo ulianza mwaka 2000 ambapo kwa mara ya kwanza uliofanyika nchini Sweden mwaka 2001.Baada ya hapo mikutano kama hiyo inafanyika kwa kupokezana kutoka Bara la Afrika na upande wa Nordic.
Dk.Mnyepe amesema kutokana na ushirikiano huo wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi hizo ,nchi hizo ziliiomba Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na uhusiano mzuri uliopo na kasi za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dk.Magufuli.
Hata hivyo alipoulizwa iwapo Tanzania itatumia nafasi hiyo kuomba nchi ya Zimbabwe kuondolew vikwazo kama ambavyo wakuu wa nchi za SADC wamekubaliana ambapo Dk.Mnyepe amesema ajenda hiyo itakuwepo kwani dhamira ya dhati.iliyopo kwa Serikali ni kuona Zimbabwe inaondolew vikwazo ilivyowekewa.
" Moja ya ajenda yetu ni kuhakikisha kila tunapopata nafasi tunaomba Zimbabwe iondolewe vikwazo, ndio msimamo wetu na ndio msimamo wa nchi za SADC.Hivyo katika mkutano huo tutazungumza na kutoa ujumbe wetu,"amesema.
Pia aliulizwa kuhusu suala la amani ambapo kuna baadhi ya nchi za Afrika usalama si wa uhakika sana, ambapo amejibu kwa sasa nchi nyingi ziko salama zikiwemo nchi jirani lakini bado iko nafasi ya kuendelea kujadiliana na ndio maana katika mkutano huo kuna nchi za Afrika ambazo haziko salama wameaalikwa na zitapata nafasi ya kusikilizwa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...