Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mtwara-Mikindani Bw.
Emanuel Mwaigobeko akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau wa zao la korosho
mkoani Mtwara iliyolenga kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za
kibiashara hususani katika zao hilo pamoja na
uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
Mmoja wa wadau wakubwa wa
Korosho mkoani Mtwara Bw Ramesh Kennedy akizungumza wakati wa hafla ya chakula
cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau hao
ili
kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao
hilo pamoja na uboreshaji wa huduma
zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
Mkuu wa huduma ya rejareja wa
benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Hazina na
Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (wa kwanza kulia) wakiwaongoza
wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Mtwara-Mikindani Bw. Emanuel Mwaigobeko
(alievaa suti nyeusi) kupata chakula wakati wa hafla hiyo.
Mtwara
; Octoba 31, 2019: Benki ya Exim Tanzania mapema wiki hii iliandaa
hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani
Mtwara ili kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani
katika zao hilo, mipango ya ukuaji na uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki
hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo
iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwemo viongozi wa
kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki
hiyo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema
kupitia hafla hiyo walilenga pia kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili
waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
“Pamoja na kushukuru kwa namna
ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya kuikuaji na ubora wa
huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao
na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Lyimo.
Alisema ukuaji wa benki hiyo
unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake na wateja wake ambao
kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo hali ambayo imekuwa
ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za kibenki ili kulinda na
kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
Pamoja na mambo mengine hafla
hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa huduma za benki hiyo
kutoka kwa wadau hao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bw. Emanuel Mwaigobeko alisema mkoa huo umejipanga kwa dhati kuhakikisha
ununuzi wa mkorosho unaenda vyema kwa kuzuia watu wachache kuharibu taswira ya
serikali pamoja na sekta nzima ya kilimo cha zao hilo.
Pamoja na kuipongeza benki ya Exim kwa namna inavyoshirikiana na wadau wa zao hilo mkoani Mtwara, Bw
Mwaigobeko alizitaka taasisi zinazohusika na masuala ya fedha mkoani humo
kusaidia katika kuwajengea uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kifedha wakulima
na wafanyabiashara wa zao hilo mkoani humo.
Alisema ni matarajio yake
kwamba wakulima watakuwa waaminifu kupeleka korosho safi ili wasiharibu ubora
wa korosho za Tanzania katika soko la ndani na nje.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...