ALIYEKUWA  rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu, wameachiwa huru kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kutupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali kupinga 
wasipate dhamana.

UPDATE NEWS


BAADA ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili, aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu hatimaye leo Novemba 5,2019 wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Washtakiwa Aveva na Kaburu wameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo walipaswa uwa na wadhamini wawili walioaini bondi ya Sh milioni 30  kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho vya taifa.

Majira ya saa  sita mchana, Kaburu pamoja na wadhamini wake walisaini fomu ya mahakama na kuachiwa huru huku Aveva akiwa anapatiwa huduma ya kwanza baada ya hali yake kiafya kuonekana kutokuwa nzuri.

Kaburu aliondoka mahakamani hapo akiwa ndani ya gari ndogo aina ya subaru yenye namba ya usajili T854 DGB.

Aveva na Kaburu wameachiwa kwa dhamana baada ya vuta nikuvute vute kati ya upande wa mashitaka na utetezi kuhusu dhamana ya washitakiwa hao, lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametupilia mbali mapingamizi ya upande wa mashitaka ya kupinga dhamana baada ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi kesi hiyo isiendelee hadi Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Simba amesema kukata rufaa kwa upande wa mashitaka hakuondoi maamuzi ya mahakama na kwamba rufaa waliyokata itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi ndio inaweza kufuta maamuzi ya mahakama ya chini.

Ameongeza kuwa,  kitendo cha serikali kukata rufaa kupitia mawakili wake hakuzuii washitakiwa kupewa dhamana hivyo maombi yao yanatupiliwa mbali.

Baada ya kutoa maamuzi hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro akisaidiana na Pendo Temu alidai kuwa anaomba kujitoa katika kesi hiyo.

Hata hivyo, Hakimu Simba aliwaeleza kuwa anaandika kwenye kumbukumbu za mahakama kwamba wamejitoa wenyewe na kuongeza kuwa sio kila wanachotaka upande wa mashitaka ni lazima kiwe hivyo na kuonya wasibishane na mahakama.

Baada ya kueleza hayo, mawakili hao wa serikali walisimama na kutoka nje ya chumba cha mahakama kwa hasira na Hakimu Simba aliwataka washitakiwa hao kuwa na wadhamini wawili na wasaini bondi ya Sh milioni 30.

Kesi hiyo imahirishwa hadi Novemba 12, mwaka huu kwa ajili ya utetezi.
Mbali na washitakiwa hao, wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka saba na kuondolewa mashitaka mawili ya utakatishaji fedha.

Katika mashitaka ya kwanza,  Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Inadaiwa Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Pia inadaiwa Aveva na Kaburu  wanadaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.Aveva anadaiwa katika benki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi. 

Aveva, Kaburu na Hans Poppe  wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli

Katika mashitaka ya nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo  kwa Levison Kasulwa  kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577


Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...