Na Woinde Shizza Globu ya jamii,Arusha
Wamiliki wa vyombo vya habari hapa nchini wametakiwa kulinda usalama wa waandishi wao pamoja na kuwajengea mazingira mazuri ya kazi ikiwemo kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili wafanyekazi zao kwa weledi
Kwa muktadha huo Usalama wa waandishi wa habari unaanzia ndani ya chombo cha habari anachofanyiakazi ambapo kinatakiwa kumuwezesha mwandishi wa habari kuanzia anavyofanya kazi pamoja na kulipa stahiki zao zote ikiwemo bima.
Hayo yameelezwa jana jijini hapa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Dk Harrison Mwakyembe wakati akifungua semina ya siku mbili ya waandishi wa habari ilioandaliwa na shirika la umoja wa mataifa la sanyansi elimu na utamaduni Unesco inayofanyika katika ukumbi wa hotel ya Four Points jijini Arusha
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa chombo cha habari kuhakikisha anamjali mfanyakazi wake katika mambo mbalimbali yakiwemo kumlipa mshahara pamoja na kumlipia bima kama kinga ya madhara yanayotokana na mazingira ya kazi .
Alibainisha kuwa iwapo mwandishi atalipwa mshahara na chombo chake cha habari ,itasaidia kuendesha maisha yake na kuacha kutegemea bahasha ambazo zinatolewa na wadau mbalimbali.
“waandishi wengi wamekuwa hawafanyikazi vizuri kwa kufuata sheria kutokana na kupewa rushwa , unakuta mwandishi anafanya habari ya uchunguzi anaianza mwanzo akikaribia kukamilisha habari yake ili aitoe anatokea mtu anamwambia nakupa fedha kiasi Fulani ili usitoe habari hii nayeye akiangalia ,chombo chake akimpi mshahara ,akimjali kwa bima wala kitu chochote anaona ni bora achukue ile rushwa na asiiandike hiyo habari kitu ambacho sio kizuri kabisa na haya yote yanasababishwa na waajiri ambao hawalipi mishahara “alisema Mwakyembe
Alibainisha kuwa Serikali aitafumbia macho swala hili na itafikia mahala itamlazimisha mmiliki wa chombo cha habari kumlipa kila mfanyakazi wake mshahara kwa mwisho wa mwezi ili kuweza kupunguza swala hili la rushwa na baasha kwa waandishi wa habari, pia serikali wanaamini kabisa iwapo mwandishi atalipwa vizuri mshahara ataweza kufanya kazi kama inavyotakiwa na ataweza kushawishiwa na bahasha zinazotolewa na wadau.
Alibainisha kuwa uandishi wa habari ni taaluma na kwa kuwa ni taaluma inatakiwa kuheshimika ,pia mwandishi wa habari ni mwalimu ambaye anafundisha jamii ,hivyo kwa kutambua hilo serikali imeamua kuweka kiwango cha elimu kinachotakiwa ili kuwezesha taaluma hii iheshimike ambapo wao kama serikali wameamua kuweka diploma kama kiwango cha kumtambulisha mwandishi .
"Hatutaki makanjanja katika fani hii kwa hiyo ndio maana serikali tumeamua kuweka kiwango hichi cha elimu pia hata hivi vyombo vyetu vya habari kukiwa na watu wengi waliosoma watakpsa watu wa kuwafanyisha kibarua na watafata watu na kuwaajiri hivyo watafata sheria"alibainisha mwakyembe
Alisema kuwa hatuwezi kuwa taifa la kuletewa tamaduni za wenzetu ,hivyo tuzingatie maadili katika jamii za Afrika na kutunza tamaduni zetu .
Kwa upande wake mkurugenzi wa Unesco Tanzania Tirso Dos Santos alisema kuwa wameamua kuandaa semina hii ya kujadili ni namna gani kama taifa litaweza kuwalinda na kusimamia haki na ulinzi wa mwandishi wa habari katika kipindi hichi ambacho mataifa mbalimbali wanakutana katika nchi zao semina hii imewashirikisha waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali
Alisema kuwa mambo mbalimbali ambayo watajadili ni pamoja na namna gani tutafanyaje kama taifa ili tuwe na mpango wa kuweza kufuafilia swala zima la ulinzi wa waandishi wa habari ,pia namna ya kupiga vita kutochukuliwa hatua kwa watu wote wanaonyanyasa au kuwatesa wanahabari wanapofanya kazi zao.
Naye wakili wa kujitegemea kutoka chama cha wanasheria Tanganyika Haroid Sungusia alisema kuwa wamekutana hapa pia kujadili namna gani watafanya kama taifa ili kuweza kulinda na kusimamia haki na ulinzi wa waandishi wa habari na kwa pamoja watoke na mpango wa kitaifa ambao utaweza kisaidia.
Alibainisha kuwa kunabaadhi ya watu wamekuwa wanavunja haki za mwandishi wa habari ,lakini katika warsha hii ya wiki moja watatoka na jibu moja ambalo litaeleza iwapo haki zake zikivunjwa basi hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa juu ya wafunjaji wa haki hizo.
Kwa upande wake mjumbe wa chama cha wahariri Tanzania Jesse Kwayu alisema kuwa waandishi wa habari na serikali wote tunafanya kazi moja ya kuhudumia wananchi hivyo ni muhimu tukashirikiana,na ikitukea sehemu serikali inafanya vyema tuisifie na pale inapokosea hatunabudi kuhikosoa .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe akifungua mkutano wa wadau wa habari jijini Arusha unaouhusu Siku ya Kimataifa ya Kukomesha uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...