Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kulia) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kushoto) Mhe. Joerg Herrera kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anasoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiwaongoza baadhi ya makamanda kutoka nchi za Tanzania,Ujerumani na Uingereza kuweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.

Baadhi ya askari wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakipokea heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Mmoja wa wapiganaji wa vita ya pili ya dunia Mzee Malagila Shimba mwenye umri wa miaka 98 akipiga saluti mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa amesimama pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kushoto) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kulia) Mhe. Joerg Herrera wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Meja Jenerali Sherrif Sheikh Othman (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Makamanda kutoka Ujerumani na Uingereza wakiwa wamesimama kutoa heshima katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeungana na jumuiaya ya Uingereza na Ujerumani Nchini na duniani kote katika kuadhimisha kumbukizi ya mashujaa waliouwawa katika vita ya kwanza na ya pili ya dunia huku ikisisitiza msimamo wake wa kuitaka jumuiya za kimataifa kuuimarisha na kuuheshimu Umoja wa Mataifa na kuheshimu sheria na taratibu za kimataifa ili kuepuka maafa kama yaliyojitikeza katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia.
Msimamo huo wa Tanzania umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia maadhimisho yaliyofayika katika makaburi ya mashujaa yaliyoko kijitonyama na baadae kuweka mashada ya maua katika mnara wa askari ulioko eneo la posta mpya jijini Dar es Salaam.
Prof. Kabudi amesema wakati Dunia ikifanya kumbukizi ya mashujaa waliouwawa katika vita ya kwanza na ya pili ni vyema hatua za makusudi zichukuliwe hivi sasa na jumuiya za Kimataifa kuhakikisha makovu,mauaji na vita vilivyotokea miaka 105 na miaka 75 ya vita vya pili vya dunia havijitokezi tena.
Ametoa wito kwa Jumuiya za Kimataifa kuuimarisha na kuuheshimu Umoja wa Mataifa alioutaja kama umoja ambao unahitajika zaidi hivi sasa kuliko miaka iliyopita ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi kwa amani na kujiletea maendeleo ya kisayansi nay a kiteknolojia.
Ameongeza kuwa ameutoa wito huo ukitilia maanani kuwa kuna viashiria ambavyo vimeanza kujitokeza kwa baadhi ya nchi duniani zimeanza kuona Umoja wa Mataifa hauna umuhimu kuanza kufanya mambo ambayo yanakwenda kinyume na sheria,kanuni na taratibu za kimataifa na kuonya kuwa hali hiyo ikiendelea huenda ikaisababisha dunia kurejea katika kadhia ya vita na madhara yake yaliyojitokeza katika vita ya kwanza nay a pili ya dunia na kwamba Tanzania inaamini Umoja wa Matifa imara unasababisha dunia yenye amani na salama.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza hapa Nchini Mhe. Sarah Cooke amesema ni bila kujali yaliyojitokeza huko nyuma kuna umuhimu mkubwa kwa dunia kuungana badala ya kugawanyika ili kuwa na dunia inayojali utu wa binadamu.
Amesema kuwa licha ya mashujaa hao kulala, ulimwengu bado haujasahau huduma waliyoitoa na kuongeza kuwa kumbukizi hiyo ya mashujaa licha ya kufanyika jijini Dar es Salaam inafanyika pia dunia kote.
Aidha,amesema tume ya makaburi ya Jumuiya ya Madola inaadhimisha vifo vya wanajeshi na wapiganaji milioni 1 nukta 7 wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola na zaidi ya makaburi ya wanajeshi na wapiganaji laki mbili na elfu hamsini kutoka katika nchi laki moja na hamsini na tatu elfu duniani kote.
Ameongeza kuwa kwa hapa Tanzania na dunia kote kuna ambao walipigana kwa kushirikiana na mataifa mengine ya ulaya na kwingineko ambapo wengi wao walifariki dunia na hivyo kuziacha familia zao wakiwemo watoto na akina mama katika maumivu.
Maadhimisho hayo ya miaka 105 ya vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 ya vita vya pili vya dunia vimehudhuriwa pia na Kaimu Balozi wa Ujerumani Joerg Herrera ambaye ameliwakilisha Taifa la Ujerumani katika eneo walikozikwa mashujaa wa kijerumani pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na wananchi.
Akizungumza mara baada ya maadhimisho hayo Kasisi Mkuu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Dar Es Salaam Padri Richard Kamenya amesema wakati tukiadhimisha kumbukumbu ya mashujaa wa vita ya kwanza nay a pili ya dunia ni vizuri kuepuka matendo yote yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...