Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAHITIMU 3237 wametunukiwa Astashahada za awali, stashahada na shahada mbalimbali katika mahafali ya kumi na nne  ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, huku wanawake wakichukua asilimia 50 ya wahitimu wote na wanaume wakichukua asilimia 46 pekee ya wahitimu wote.

Akizungumza katika mahafali hayo Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Stephen Wasira amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi bora wa uzalendo na uadilifu katika jamii na kueleza kuwa Chuo hicho ni tunu na hazina kubwa nchini hivyo ni vyema wahitimu hao wakajitofautisha kwa kuweka mbele maadili uzalendo.

Wasira amesema, Tangu Chuo hicho kianzishwe mwaka 1961 viongozi na wengi kutoka taasisi za umma na binafsi wamepitia mafunzo kutoka katika Chuo hicho, na amezishauri taasisi  kuendelea kupata maarifa katika Chuo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho  Profesa.Shadrack Mwakalila amesema kuwa chuo hicho kinaendeleza dira ya kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kutoa maarifa bora na elimu kuhusiana na ubunifu na uvumbuzi pamoja na kuendeleza amani na umoja wa kitaifa.

Prof. Mwakalila amesema wanatumai kuwa wanafunzi hao ambao idadi ya wanawake ni 1735 na wanaume 1502 watakuwa mstari wa mbele kwa kuwa wazalendo na kuwa na maadili yatakayoigwa na watanzania.

Amesema kuwa Chuo kimejipanga kuwa kitovu cha mafunzo ya uongozi na maadili na tayari wameanza na mkakati wa kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi, maadili na utawala bora kwa sekta za Umma na binafsi kwa ngazi zote kuanzia Kijiji, Wilaya na Kata.

Prof. Mwakalila amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwaka 1961 bado kinandelea kutoa mafunzo kwa viongozi chipukizi ili wawe wazalendo na wenye maadili hapo baadaye.

Akizungumza malengo ya chuo hicho kwa sasa Prof. Mwakalila amesema kuwa wapo katika mchakato wa kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia, kuongeza maktaba pamoja na kuongeza udahili kwa wanafunzi.

Aidha ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na chuo hicho na amewasihi wahitimu hao kutumia vyema maarifa waliyoyapata na kuwa wazalendo wa mfano katika jamii zao.
 Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira(kushoto) katika maandamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya kumi na nne ya Chuo hicho kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira akikiwa na viongozi wa Chuo wakati wa mahafali ya kumi na nne ya Chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...