Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TUME
ya Ushindani Tanzania (FCC) kwa kushirikiana na Mamlaka za EWURA,
LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku
ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 5 kila mwaka na mwaka
huu itaenda sambamba na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi
kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na
maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya
ushindani nchini (FCC), Profesa. Humphrey Moshi amesema Tanzania imekuwa
ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 na kwa mwaka huu
maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya
kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani
Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."
Amesema
kuwa kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Desemba 5 na Waziri
mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa atakuwa mgeni
wa heshima.
Prof.
Moshi amesema kuwa mitandao imekuwa ikikuza biashara kama ikitumiwa
vizuri, "Biashara mtandao ni ile inayohusisha mabadilishano ya taarifa
kupitia mtandao wa kompyuta, kimsingi ni jambo zuri kwa kuwa tafiti
zinaonesha kuna masoko ya kutangaza bidhaa kwa urahisi hata kwa kuvuka
mipaka ukilinganisha miaka iliyopita" ameeleza .
Vilevile
amesema kuwa lazima jamii itambue fursa za masoko ya mtandao licha ya
kuwepo na baadhi ya changamoto,lakini tume hiyo itaendelea kuhakikisha
inawezesha masoko na kuwasiliana kwa urahisi, na hiyo ni pamoja na
kuimarisha mifumo na uwezo wa biashara.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani nchini Godfrey Machimu
amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahusisha maonesho mbalimbali
kutoka kwa wadau pamoja na kupata fursa ya kujua utendaji kazi wa
Mamlaka hizo.
Machimu
amesema kuwa Tume ya Ushindani kupitia maadhimisho hayo wanaamini
italeta chachu katika kutatua changamoto za biashara mtandao
zinazowakabili wananchi kote nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Godfrey Machimu akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani),leo jijini Dar akieleza kuhusu tume
hiyo ikishirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA
na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo
huadhimishwa Desemba 5 kila mwaka,ambapo mwaka huu itaenda sambamba na
kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya
kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja
na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.
Mkurugenzi
wa Utafiti na Muungano wa Makampuni na Urabishi Dkt. Allan Syril Mlulla
akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari namna maadhimisho hayo
adhimu kwa Wadau yatakavyofanyika sambamba na kutoa elimu na kueleza
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Ushindani Prof. Humphrey Moshi akizungumza mbele ya
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar, kuhusu namna
Tanzania ilivyojiandaa kuadhimisha siku hiyo,amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 ,lakini kwa
mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na
masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha
Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao." 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. Picha na Michuzi JR.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. Picha na Michuzi JR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...