Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameieleza Mahakama ya Halimu Mkazi Kisutu kuwa hakuwepo kwenye maandamano ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakielekea kwenye ofisi za msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni.

Mbowe alidai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati akitoa utetezi wake dhidi ya masgtaka yanayomkabili.

Akingozwa na wakili wake Peter Kibatala Mbowe alidai kuwa kama alitajwa katika mashtaka hayoya kukataa kutawanyika basi ilikuwa ni kwa hisia kwa sababu hakuwepo eneo la tukio.

Alidai kuwa baada ya kumaliza mkutano wa kufunga kampeni katika uwanja wa Buibui Mwanyamala aliindoka uwanjani hapo akiongozwa na askari polisi kuelekea Makao Makuu ya Chadema Kinondoni.

Alidai siku hiyo wahudhuriaji wa Chadema wakiwa njiani walikutana na wahudhuriaji wa CCM katika makutano ya barabara ya Morocco na Mwananyamala wakiwa na mgombea wao wakisindikizwa na ngoma aina ya mdundiko.

Mbowe alidai kuwa wanachama hao wa Chadema walikuwa wakiongozwa na Polisi kuelekea barabara ya Morocco ambapo yeye hakujua kilichoendelea nyuma kwani aliendelea na safari yake ya kuelekea Makao Makuu ya Chadema.

Akizungumzia kufikishwa kwake Mahakamani Mbowe alidai kuwa kwa mara ya kwanza alipokea wito wa kuitwa Polisi kupitia mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Alidai kuwa Kamanda huyo wa Polisi alitoa wito kwa viongozi wa Chadema kuripoti polisi kuhusiana tukio hilo la maandamano.

Pia alidai kuwa alipata taarifa kuhusu kifo cha Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi katika maandamano hayo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari na kwamba Polisi inawashilikia askari kuhusu tukio hilo.

Mbowe alidai kuwa hajawahi kula njama na washtakiwa wenzake bali waliitwa kwa nyakati tofauti kwenda Polisi.

Mbali na Mbowe washitakiwa wengine  katika kesi hiyo,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na  Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini,  Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...