Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
ABIRIA
waliokuwa wakisafiri na basi la Majinja lenye namba T 619 DCF
wamenusurika kifo baada basi hilo kupata ajali katika eneo la Mlima
Kitonga mkoani.
Ajali
hiyo imetokea leo na kusababisha taharuki waliokuwa wakisiri na basi
hilo ambapo hata hivyo baadhi ya abiria wamepata majeraha na hakuna
aliyepoteza maisha kutokana na ajali hiyo.
Wakizungumza
na Michuzi TV na Michuzi Globu ya jamii, baadhi ya mashuhuda wa ajali
hiyo wamesema baada ya kutokea kwa ajali hiyo walitoa msaada wa kuwatoa
abiria waliokuwa ndani ya basi hilo.
Baadhi
ya abiria wametolewa kupitia madirishani kutokana na kwamba basi hilo
kilikuwa limepinduka kwa magurudumu kuwa juu na paa la basi kuwa chini.
Kwa
mujibu wa mashuhuda hao walioamua kutoa msaada kwa abiria hao, wamesema
jambo la kushukuru Mungu ni kwamba hakuna aliyepoteza maisha ila kuna
baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo.
"Kwa
kweli tunashukuru hakuna aliyepoteza maisha katika ajali
hii,tumefanikiwa kuwatoa wote waliokuwa ndani ya basi la Majinja.Ila
kuna baadhi ua abiria wamepata majeraha.
"Kwa
sasa tunawaona wako vizuri sijui labda kama kutakuwa na abiria ambaye
amepata majereha kwa ndani,"amesema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Hata
hivyo Michuzi Globu na Michuzi TV inaendelea kumtafuta Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Iringa ili kuzungumza ajali hiyo na hali za majeruhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...