Na, Editha Edward-Tabora
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Wilayani Igunga mkoa wa Tabora imewakamata viongozi sita wa chama cha Msingi cha Wakulima wa zao la pamba AMCOS wa kijiji cha Choma na kuwafikisha mahakama ya hakimu Mfawidhi wilaya ya Igunga kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wakulima
Kwa upande wa muendesha mashitaka wa taasisi hiyo Mazengo Joseph aliiambia mahakama mbele ya hakimu Lydia Ilunda kuwa washitakiwa wote walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 15 (1) a (2) na 3 (a) sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na 11 ya 2007
Waliofikishwa Mahakamani mwishowa wiki hii iliyopita ni. Mwenyekiti wa baumu AMCOS , Nyolobi Nangale (36), Sylvester Masanyigule (46), Andrew Senga(49), Iwize Masanja(37) Elias Kelege (25), Martine Silas (31) wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha choma
Muendesha mashitaka Mazengo Joseph amesema kuwa washitakiwa wote wanakabiliwa na mashitaka matatu shitaka la kwanza, kati ya agosti 1 mwaka huu na Oktoba 25 mwaka huu kwa muda tofauti katika kijiji cha choma, washitakiwa wote kwa pamoja waliomba rushwa ya shilingi laki nane kutokea kwa kulwa Mabula ili waweze kumlipa fedha zake za pamba shilingi milioni nane laki tatu arobaini na tano elfu miambili Ishirini alizokuwa ameiuzia pamba kampuni ya OLAM
Shitaka la pili linalowakabili washitakiwa wote katika tarehe hiyo na muda tofauti waliomba rushwa ya shilingi laki sita kutoka kwa Shimbi Ganja ili waweze kumlipa fedha zake shilingi 6,536,400 alizokuwa ameuza pamba kwenye kampuni ya OLAM
Shitaka la tatu amesema katika tarehe hiyo na muda tofauti waliomba rushwa ya Shilingi laki sita kutoka kwa Shimbi Kadengu ili waweze kumlipa fedha zake Shilingi milioni 6,220,680 aliyouza pamba kwa kampuni ya OLAM
Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka hayo waliyakana yote ambapo kesi hiyo imehairushwa hadi novemba 6 mwaka huu itakapotajwa tena ambapo washitakiwa wawili wamedhaminiwa kwa dhamana yq shilingi milioni tano mmoja huku wanne wakipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...