Na Chalila Kibuda,Globu Jamii
VIJANA wameaswa kuwa na maarifa katika kujiimarisha katika kuanzisha Kampuni au Biashara katika kutatua tatizo la ajira.
Hayo wameyasema wadau katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na My Legacy ikishirikiana na Viva Legacy kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika masuala ajira na kuanzisha Kampuni au ujuzi wa kufanya ubunifu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu amesema serikali imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vijana wanaondokana na changamoto ya ajira .
Amesema kuwa tatizo la ajira ni ukosefu wa maarifa hivyo vijana hao wakiwa na maarifa watakuwa na uwezo wa kuingia katika sekta ya Viwanda na kutatua tatizo la ajira.
Dkt.Semakafu amesema kuwa vijana wanatakiwa kufungua mawazo ajira badala ya kufikiria kuajiriwa.
Aidha amesema kuwa kumekuwa na mahusiano na sekta binafsi katika kuhusianisha masuala ya ajira ili vijana wengi waingie katika sekta hiyo kwa kuanzisha Kampuni au Biashara ili kuajiri baadhi ya vijana.
Amesema kuwa ni wakati kujipanga pamoja katika kuelekea uchumi wa kati kuhamasisha vijana kuingia katika uchumi wa viwanda kwa kuanzisha Kampuni au Biashara.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Viva Legacy, Fortunata Temu amesema kuwa kutakuwa na programu ya kutoa mafunzo kwa vijana katika kuchambua mawazo ya namna ya kufungua milango ya ajira kwa kuanzisha Kampuni au Biashara.
Temu amesema kuwa vijana kwa pamoja wakiweza kutumia mafunzo hayo watafanikiwa ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi wa sekondari kutambua kuhusiana changamoto ya ajira.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema kuwa vijana wanaohitimu kwa mwaka ni 1200,000 wanaoingia katika ajira ni 500000 hadi 600000 wengine wanakosa ambao wanatakiwa waingie katika sekta binafsi kwa kuanzisha Kampuni au Biashara.
Amesema kuwa waajiri katika nchi hii ni wachache ikilinganishwa na vijana wanaohitimu na wanatakiwa kuajiriwa.
Simbeye amesema wakati mwingine sekta binafsi kwa vijana kuingia ni ngumu kutokana Mazingira ya kuwepo kwa tozo nyingi.
Hata hivyo amesema serikali inatakiwa kuwepo na sera kwa vijana wakianzisha Biashara kuacha kuchukua kodi ili waweze kuzalisha.
Naibu Katibu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave maria Semakafu akizungumza na waaandishi wa habari kuhusiana na kongamano la vijana kuhusiana na ajira lililoandaliwa na Viva legacy lilofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza katika kongamano la vijana kuhusiana na nafasi ya sekta binafsi katika kuweza kujiajiri katika kongamano lililoandaliwa na Viva Legacy jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Viva Legacy, Furtunata Temu akizungumza namna walivyojipanga katika kutoa mafunzo kwa vijana kukabiliana na tatizo la ajira katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye kongamano lililoandaliwa na Viva Legacy jijini Dar es Salaam.
Naibu katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akifuatilia mada katika kongamano la vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...