Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka amesema kuwa wakazi katika vijiji Wilayani humo wameanza kuchimba matundu vyoo kutekeleza Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mwinuka amesema wananchi wamekubaliana kuchimba matundu ya vyoo 50 kwa shule za msingi Ruvuma na Mihambwe
Katika Kijiji Cha Chitoholi na Mkupete tayari nao wameanza ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Chitoholi na Mkupete
"Tupo pamoja katika Kampeni ya shule ni choo ambapo wananchi wamekubaliana kujenga matundu ya vyoo katika shule zao za msingi kwa kujitolea kwa Hali na Mali ili tatizo Hilo lisiwepo katika maeneo yao,"alisema Mwinuka
Kampeni ya shule ni choo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa la kuondoa tatizo la uhaba wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari ndani ya Mkoa wa Mtwara
Ujenzi wa Matundu ya vyoo ukiendelea
Wanakijiji wakijitolea katika maandalizi ya kujenga matundu ya vyoo
Wanakijiji wakijitolea katika maandalizi ya kujenga matundu ya vyoo
Wananchi wakijadiliana ili kufikia malengo yao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...