Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa akiwaonyesha wanahabari(hawapo pichani ) panga na msumeno alivyokutwa navyo, bwana Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp.
********************************
Na Farida Saidy morogoro
Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro linamshilia Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo na alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji yaliyokuwa yakitiririka kwa kasi kabla ya kukamatwa na askari Polisi.
Video clip ya tukio hilo la aina yake ilitembea kwa kasi katika mitandao ya jamii kutwa nzima jana na leo, japo awali maelezo yalisema kuwa imetokea maeneo ya Mbweni.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa Askari wake walipokea taarifa toka kwa raia mwema juu ya uwepo tukio hilo na baada ya kufika eneo la tukio ambapo ni eneo la chanzo cha maji wakamkuta mtuhumiwa akiwa na Mtoto wake, wote walikua uchi wa mnyama.
Aidha katika Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno ambapo pia kunadaiwa kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo Mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa Kihonda, ambae nae anasema muwewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo yasiyoeleweka na kwamba siku hiyo ya tukio aliaga anaenda kuogelea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...