Dar es Salaam, 20 Disemba 2019:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi pamoja na kanda ya kati zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya nchi. Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea zaidi katika maeneo hayo. 
Hivyo, tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa kwa siku ya kesho tarehe 21/12/2019 inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. 
Aidha, kwa tarehe 22/12/2019 vipindi hivyo vya mvua kubwa vinatarajiwa kupungua. Hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa Angalizo la mvua kubwa. 
Kutokana na uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa kaskazini mashariki mwa Madagascar TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini. 
USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua.
Imetolewa na; 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. 
Mawasiliano yote yaelekezwe kwa:
Mkurugenzi MkuuMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Morogoro Rd, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3
S.L.P. 3056, Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8 Barua pepe: met@meteo.go.tz, Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga) 
105A – 09/19 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...