Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Hussein Bashe akiongea na Wanahabari katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma leo, wengine ni Wakuu wa Taasisi, Wakurugenzi wa Bodi za Mazao na Wakala mbalimbali zilizochini ya Waizara ya Kilimo


Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe leo ametangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa miundombinu ya Kituo cha Kusafirisha Mazao kwenda nje ya nchi kupitia Bandali ya Dar es Salaam na kuwataka Wadau wote wa mazao ya kilimo kupeleka mahitaji yao na viwango wanavyotaka ili kuiwezesha Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji na Mauzo Nje ya Nchi (EPZA) ianze kujenga kulingana na mahitaji ya kila zao.

Akiongea na Wanahabari katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, Jijini Dodoma, Waziri Bashe amesema, kuanzia leo Wadau wote wa mazao ambayo yatakuwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi wanapaswa kupeleka mahitaji yao pamoja na viwango (Specifications) ili ujenzi uanze.

“Napenda kuwafahamisha Wadau wa mazao ya kilimo ambayo yanasafirishwa kwenda nje ya nchi kupeleka mahitaji yao kwa (EPZA) ili waanze kujenga kulingana na mahitaji ya kila Mdau.”

“Kila zao lina upekee na mahitaji, yanatofautiana, mwengine atahitaji majokofu, mwengine atahitaji tu ghala la kuhifadhia tu mazao na mwengine atahifadhi na kuweka kwenye madaraja na kuyafunga kwenye vifungashio (Park House). Amekaririwa Mhe. Bashe.

“Napenda kuwafahamisha Watanzania kuwa mazao kama chai, yataanza kusafirishwa Kurasini Dar es Salaam na ndiyo itakuwa “One Stop Centre” ya kusafirishia mazao mengi, mfano chai, matunda na mbogamboga”. Amemalizia Waziri Bashe.

Kunaza kwa mchakato huo ni jibu la kilio cha Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya kilimo kwa muda mrefu na kwamba kuanza kwa mchakato huo wa ujenzi wa Kituo cha Kuuza na Kusafirisha Mazao kwenda nje ya nchi (Kurasini Agro Logistic Hub) kutarahisisha biashara ya mazao kwenda nje ya nchi.

Naibu Waziri Bashe ameongeza kuwa zoezi hilo linaenda sambamba na ujenzi wa Ofisi za Taasisi nyingi za Serikali ambazo zinahusika moja kwa moja na usafirishaji wa mazao kwenda nje ya nchi; Taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), Wizara ya Kilimo (Afya ya Mimea) Mamlaka ya Bandari (TPA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...