Na Irene Mwidima, Yassir Simba - Globu ya Jamii.
Serikali imezipongeza taasisi za SIDO, Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, taasisi za vijana na halmashauri kwa kushirikiania vyema na Shirika lisilo la kiserikali la kusimamia haki za mtoto wa kike nchini (CAMFED) katika kuwawezesha vijana hasa wasichana kupata fursa zinazotolewa na shirika hilo.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa, jijini Dar-es-salaam, Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, amesema kuwa mkutano huo unatoa fursa ya kupata mrejesho wa utekelezaji wa mipango mkakati wa CAMFED 2015 - 2019 pia kujadiliana na kupata maoni yatakayoboresha mpango mkakati wa shirika kwa miaka mitano ijayo.
Amesema kwamba ni matumaini yake kuwa taasisi za serikali pamoja na wadau wa mkutano huo watatumia fursa hizo kuishauri vyema CAMFED ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mikakati ya kuwasaidia wasichana kupata fursa mbalimbali kama za ajira, elimu, mikopo ya vijana serikalini, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya ufundi na ujuzi ili waweze kufikia malengo yao.
Ameongeza kwa kusema "Niwapongeze pia kwa kuanzisha elimu ya stadi za maisha katika shule za sekondari. Elimu hii imewezesha wanafunzi kujitambua, kuboresha ustawi wao na kufahamu, kuboresha mahudhurio na kupunguza utoro mashuleni".
Kwa upande wake mkurugenzi wa CAMFED, Lydia Wilbard ametoa wito kwa wazazi kushirikiana kikamilifu kuhakikisha suala la uwezeshaji wa elimu kwa watoto wa kike katika jamii zao na kukemea vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia miongoni mwa watoto wa kike katika jamii.
Pia amesema kuwa CAMFED inasimamia sera ya ulinzi wa mtoto kwa kusimamia haki za mtoto, na kunahamasisha ushiriki wa jamii katika kuboresha miundombinu ya kufundisha na kujifunza shuleni ikiwemo utoaji wa chakula, vifaa vya shule kwa wanafunzi, kuboresha miundombinu kama madawati, vitanda, ukarabati wa mabweni ya wasichana na nyumba za walimu, hii imechangia kuongeza uelewa kwa jamii katika utekelezaji wa waraka wa elimu bila malipo.
Kaimu mwenyekiti wa CAMFED, Bw. Msigwa yeye azungumzia kuhusu hali halisi ya maendeleo ya CAMFED katika mikoa iliyofikiwa na shirika hilo na kueleza ya kwamba maendeleo ni mazuri na bado wanapiga vita vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, pia kuisaidia mikoa ambayo haijafikiwa na shirika hilo.
Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa Mwaka wa Shirika lisilo la kiserikali la kusimamia haki za mtoto wa kike nchini (CAMFED), uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam
Picha zote na Al Hassan Muhidin.
Picha zote na Al Hassan Muhidin.
Baadhi ya waalikwa na wanafunzi waliohudhulia Mkutano huo, wakifatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa CAMFED, Lydia Wilbard.
Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Bodi ya CAMFED, baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...