Picha ya pamoja
Katibu MKuu wa CCM,Dkt Bashiru Ally akifafanua jambo mbele ya wageni wake (hawapo pichani),wakati wa Mazungumzi yao na Balozi wa China
Kikao kikiendelea
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally leo amefanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke ambapo ametaka fursa zinazotolewa kwa watanzania kusoma vyuo vya nje zijikite katika teknolojia ya uzalishaji.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu Dodoma pamoja na mambo mengine, yamelenga katika kupanua wigo wa ushirikiano ambapo Dkt. Bashiru ameleeza msimamo wa CCM kuhimiza zaidi kupatikana kwa fursa zenye tija kwa maendeleo ya viwanda hasa zinazolenga mafunzo ya vitendo katika kilimo, ufugaji na viwanda.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...