BAADA ya kupata uongozi mpya Kampuni ya SimbaNET nchini imejipanga kwa dhamiria ya kutoa suluhisho ya ubunifu kwa kupunguza gharama zake kwa bei nafuu kwa wateja wake na kuhakikisha wanawafikia wateja wengi zaidi.
Kauli hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari baada ya kumtangaza rasmi,Meneja Mkazi nchini Tanzania wa Wananchi Group kupitia Kampuni hiyo,Sanctus Mtsimbe huku Kennedy Ojungouya akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo na kuwa
Mkurugenzi Mkuu kwa masoko wamasuala ya mawasiliano wa Mwananchi Group.
Imefafanuliwa kuwa kampuni hiyo inatoa huduma tofauti tofauti katika nchi nyingi barani Afrika na kwamba miongoni mwa baadhi ya nchi zilizokuwa zinafanya kazi na kampuni hiyo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Malawi, na Zambia.
Aidha katika taarifa hiyo imesema Mtsimbe amepitia katika uongozi mbalimbali ikiwemo Ofisa Mwandamizi wa SimbaNet Afrika Mashariki .Pia tayari aliwahi kuwa na nafasi ya Meneja Mkuu wa Teknolojia ya Mawasiliano ya Airsys (Uingereza) na Meneja Mauzo wa Mkoa kwa Mawasiliano ya Danimex ya nchini Denmark.
Wakati kwa upande wa Ojungouya imeelezwa ana uzoefu mkubwa katika tasnia ya mawasiliano baada ya kufanya kazi katika uwezo wa juu wa mashirika anuwai ya kimataifa.
Aidha kikundi cha wananchi hutoa ufanya biashara mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya makazi, mtandao na huduma za burudani na huduma za mawasiliano ya biashara .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...