Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
umeme Tanzania(TANESCO) na mwenyekiti wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi
wa Tanesco, Dkt Tito Esau Mwinuka akifafanua jambo katika mkutano wa
baraza hilo uliofanyika Mkoani Morogoro leo disemba 11,2019.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Morogoro leo disemba 11,2019.
……………………….
Na Farida Saidy Morogoro
Hali ya upatikanaji wa umeme
nchini imezidi kuhimlika ambapo kwa sasa mfumo wa gridi ya taifa una
wastani wa zaidi ya megawati 200 kwa siku wakati mahitaji ya juu ya
umeme yamapanda kufikia megewati 1120 mpaka kufikia Novemba 2019.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO na mwenyekiti wa baraza kuu, Dkt Tito Esau Mwinuka
katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa Tanesco
leo disemba 11,2019.Mkoani Morogoro ambapo amesema kuwa hali ya
utendaji na kasi ya utoaji huduma ndani ya shirika imezidi kuboreka
ikiringanisha na hapo awari.
Katika hatua nyingine Dkt Mwinuka
amesema kuwa mradi wa power reliability enhancement program( POREP
)Utasaidia kuhakikisha miundombinu ya usambazaji umeme inafanyiwa
matengenezo,na kuondoa kero ya kukatika katika kwa umeme,hivyo utasaidia
kuokoa mapato ya yanayopotea kutokana na kukatika mara kwa mara kwa
umeme.
Aidha makusanyo ya fedha za ndani
yamepanda ukilinganisha na hapo awari ambapo kwa mwezi oktomba 2019
shilingi bilioni 160.4 zimekusanywa huku oktoba 2018 shilingi bilioni
155.9 zilikusanywa,hata hivyo shirika linadaiwa shilingi bilioni 952
ambapo lipo katika mikakati ya kuweza kulipa deni hilo.
Kwa upande wake Mhe Mwalimu
Mohamed Utaly Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ambaye pia amemwakirisha Mkuu wa
Mkoa wa Mrogoro Mhe Loata Sanare akifungua mkutano huo amelipongeza
shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kazi kubwa inayoifanya ya
kusambaza na kuunganisha umeme kwa wananchi wa mijini na vijijini.
Hata hivyo amelitaka shirika
kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kukatika kwa umeme mara kwa
mra,ambpo amesema kukatika kwa umeme kunasababisha hasara kubwa kwa
watanzania hususani wenyevinda na vikubwa vidogo .
Mkutano huo unaketi mkoani
morogoro kwa siku tatu ambapo umefunguliwa na mkuu wa wilaya ya mvomero
ambaye amemwakilisha mkuu wa Mkoa Wa Morogoro Mhe Loata Sanare na
kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo,Paul Sangeza Mwenyekiti wa
TUICO, Mhandisi Elangwa Mgeni Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco ya
kujenga na kurekebisha miundombinu ya umeme (ETDCO).
Wengine ni Shairu Idrissa
mwakirishi wa Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco inayoshughurika na
utafiti wa uzarishaji umeme kutumia joto ardhi (TGDC)mhandisi yusuphy
kitivo kaimu meneja mkuu wa kampuni tanzu ya tanesco inayoshughurika na
utengenezaji wa nguzo za zege (TCPM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...