Anaandika Abdullatif  Yunus wa Michuzi TV.

Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, na Miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kwa kufanya shughuli za Kijamii ikiwemo usafi wa Mazingira na Uchangiaji wa Damu, ikiwa ni kumbukumbu ya Sherehe ambazo hufanyika Desemba 9 ya kila Mwaka.

Shughuli hizo zimefanyika mapema Desemba 4, 2019 kwa kuishirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, pamoja na watumishi na watendaji wa Serikali, shughuli hizo zikianzia Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  kuelekea Barabara ya Soko Kuu Bukoba, ambapo umefanyika Usafi kuzunguka maeneo yote ya Soko hilo, na kisha kuelekea Hospitali ya Rufaa Mkoa Kagera kwa ajili ya Uchangiaji Damu.

Akizungumza na wananchi na Wafanyabiashara Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amezidi kuwakumbusha umihimu wa kufanya Kazi kwa bidii na ubunifu ili kuongeza chachu ya Uchumi, kuwa wazalendo wa Taifa, na mara nyingi akizidi kuwakumbusha mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ndani ya Miaka minne Mkoani Kagera ikiwemo yaliyofanywa katika Sekta ya Afya, Elimu, Utalii, Kilimo na Miundo mbinu ikiwa ni pamoja na Ujenzi na Ukarabati wa Meli Mpya itayosaidia urahisi wa biashara zao.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameongoza kuwa watumishi wengine katika zoezi la kujitolea Uchangiaji Damu, lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera sambamba na kutembelea baadhi ya maeneo ya Hospitali  wodi ya akina mama, na kushuhudia ujenzi wa Wodi hiyo inayoendelea kujengwa.

Akiwa Hispitalini hapo amewasihi bodaboda kuendelea kufuata na kutii sheria za barabarani kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza ajali ambazo hupelekea mahitaji makubwa ya Damu.

 Pichani shughuli za Usafi zikiendelea maeneo mbali mbali ya Soko Kuu la Bukoba katika uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kwa Mkoa Kagera.
 Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akionekana kushiriki zoezi la Uchangiaji Damu, mapema Desemba 04, 2019 katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kimkoa.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara Mara baada ya kumalizika shughuli ya Usafi katika uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kwa Mkoa Kagera
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...