KUSUASUA kwa ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso, Mkoani Mbeya unaotekelezwa na mkandarasi Lukolo Construction Company umepelekea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako kutoa agizo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kusimamia kwa karibu ukamilishaji wa kazi hiyo ili majengo hayo yaweze kutumiwa na walimu tarajali.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua mradi huo na kukuta ukitekelezwa kwa hali isiyoridhisha na katika baadhi ya maeneo kuwa chini ya kiwango.

Amesema mkandarasi huyi pamoja na kushindwa kukamilisha kazi yake kwa wakati aliepewa muda zaidi ili kukamilisha kazi hiyo lakini bado hajakamilisha hivyo kupelekea chuo kushindwa kutumia miundo mbinu na Serikali kuchelewa kufikia malengo yake ya uboreshaji na upanuzi wa Chuo hicho.

"Naelekeza mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 30 tena kwa ubora kama ilivyopangwa hivyo Katibu Mkuu afuatilie kwa karibu kazi hii na makandarasi akishindwa kukamilisha mchukulie hatua," amesema Ndalichako

Kiongozi huyo alisema kwa mujibu wa makubaliano mapya baada ya kurudishwa kazini ni kukamilisha kazi hiyo Desemba 30, 2019 lakini hata sasa haonekani kuwepo eneo la mradi na hakuna kinachoendelea.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mbeya Albert Chalamila amemweleza waziri kuwa mkandarasi huyo asipokamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa atachukuliwa hatua na kuwa kama Mkoa watafuatilia pia utekelezaji wake kwa karibu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pia amemwomba waziri wa elimu kukipatia Chuo hicho gari ili kusaidia katika huduma mbalimbali jambo ambalo Waziri aliridhia na kusema kuwa tayari Wizara imenunua magari kwa ajili ya vyuo vya ualimu ambavyo havina huduma hiyo.

Nae mkuu wa chuo cha ualimu Mpuguso Dorothy Mhaiki ameishukuru Serikali kwa namna inavyoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika chuo hicho na kuomba kukarabati maeneo mengine yaliyobakia kwa kuwa bado kuna uhitaji ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana watumishi wa kudumu Upande wa walinzi na wapishi ili kupunguza gharama ya uendeshaji.

Ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika Chuo hicho ambao umegharimu kiasi cha sh bilioni 10 unaotekelezwa na serikali ya Tanzania na ile ya Canada.

Mradi huo umetekelezwa na kandarasi mbili Salem Construction Ltd ambao wamekalilisha kazi zao kwa ubora na majengo kuanza kutumika na Lukolo Construction Company ambao bado kazi yao haijakamilika.

Nyumba za walimu zilizojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kukamilika kwa ubora


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce  Ndalichako akikagua mlango  uliowekwa katika moja ya jengo linalojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ambao uko chini ya viwango.
 Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Ualimu  Mpuguso Wilayani Rungwe Dorothy Mhaiki alipowasili chuoni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi unaotekelezea Chuoni hapo.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila wakikagua moja ya jengo lenye madarasa linalojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso Tukuyu Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...