NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa amesema ,mwaka 2019 makosa
ya jinai yamepungua kwa asilimia 10.5 na kuongeza kwamba hali ya
usalama kijumla ni shwari.
Aidha
amesema, makosa ya kukutwa na silaha na risasi walikamata jumla ya sila
17 ikiwa ni pamoja na SMG moja na magobore 16 na risasi sita za SMG
huku watuhumiwa 20 walifikishwa mahakamani kutokana na makosa hayo.
Aliweka
bayana hayo wakati akielezea namna walivyojipanga kudhibiti masuala ya
uhalifu wakati wa sikukuu ya krismas na mwaka mpya.
Wankyo,
alieleza yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi ni 2,074 ukilinganisha
na mwaka 2018 ambapo makosa yalikuwa 2,318 hivyo yamepungua kwa makosa
244.
Alisema,
kati ya makosa hayo makosa ya jinai dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji
,kubaka ,kulawiti mwaka uliopita yalikuwa makosa 382 ,na mwaka huu
yameripotiwa makosa 366 hivyo yamepungua 16 sawa na asilimia 12.
"Makosa
ya kuwania mali kama vile unyang'anyi na kutumia silaha,unyang'anyi wa
kutumia nguvu ,wizi wa silaha ,uvunjaji nayo yamepungua makosa 236 sawa
na asilimia 19,kutoka makosa 1,240 mwaka 2018 hadi kufikia makosa 1,004
yalitokea mwaka huu"alifafanua.
Kamanda
huyo alibainisha, jeshi hilo pia lilizuia magendo na uhalifu katika
bandari bubu ,na kukweps ushuru zilikamatwa mafuta ya kupikia madumu
5,260 ,khanga balo 16,matairi ya pikipiki 175, mafuta ya diezel lita 320
yalikamatwa huku watuhumiwa 23 walifikishwa mahakamani.
Hata
hivyo Wankyo,aliwataka wananchi washeherekee sikukuu kwa amani na
utulivu na kuyataka magari yasijaze abiria kupita kiasi na madereva
wafuate sheria za usalama barabarani pasipo kulewa wala kuendesha kwa
mbwembwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...