BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini NBAA, imepitisha na kutangaza matokeo ya watahiniwa 6179 waliofanya mtihani kati ya Oktoba 29 hadi Novemba, 2019 katika ngazi mbalimbali za masomo.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.
"Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,805 kati ya hao watahiniwa 626 sawa na asilimia 9.2 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 6,179 sawa na asilimia
90.8. Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 237 ambao ni asilimia 3.8 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 41 sawa na asilimia 0.7 wamefaulu kwa kufaulu masomo walioyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 921 sawa na asilimia 14.9 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza," alisema Maneno.
Pia alisema watahiniwa 1,199 sawa na asilimia 19.4 wamefaulu mitihani yao na kwamba watahiniwa wengine 2,678 sawa na asilimia 43.3 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali na watahiniwa 2,302 waliobakia sawa na asilimia 37.3 hawakufaulu mitibani yao.
Awali, taarifa hiyo ilieleza kuwa watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 765 kati ya hao watahiniwa 77 sawa na asilimia 10.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo kufanya ndani ya watahiniwa waliofanya mitihani kuwa 688 sawa na asilimia 89.9.
Pia imeelezwa kuwa kati ya watahiniwa 688 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 135 ambao ni asilimia
19.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku wengine 04 sawa na asilimia 0.6 wamefaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 168 sawa na asilimia 24.4 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza.
Imeelezwa kwa ujumla watahiniwa 307 sawa na asilimia 44.6 wamefaulu mitihani yao na watahiniwa 255 sawa na asilimia 31.7 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 126 waliobakia sawa na asilimia 18.3 hawakufaulu mitihani yao.
Aidha, katika hatua ya Kati, waliojisaliwa walikuwa 3,685 kati ya hao watahiniwa 375 sawa na asilimia 10.2 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 3,310 sawa na asilimia 89.8. Kati ya watahiniwa 3,310 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 33 ambao ni asilimia
1.0 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 31 sawa na asilimia 0.9 wamefaulu kwa kufaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Alisisitiza kuwa asilimia 12.4 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, hivyo Kwa ujumla watahiniwa 474 sawa na asilimia 14.3 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 1,529 sawa na asilimia 46.2 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 1,307 waliobakia sawa na asilimia 39.5 hawakufaulu mitihani yao.
Katika hatua ya mwisho, watahiniwa 337 sawa na asilimia 15.7 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 784 sawa na asilimia 40.8 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 802 waliobakia sawa na asilimia 41.7 hawakufaulu mitihani yao.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.
Alisema mitihani ya katikati ya muhula kwa ajili ya masomo ya A5 Business Law, B5 Performance Management, C3 Corporate Finance and C4Advanced Taxation itafanyika Februari 25 na 26 2020 katika kituo cha Dar es Salaam hivyo, wanaopenda kujisajili katika mitihani hiyo wanakaribishwa.
"Mahafali ya 42 ya NBAA yatafanyika Oktoba 3, 2020. Tangazo rasmi kuhusu mahafali hayo litawekwa kwenye tovuti ya bodi. Wale wote waliofaulu mitihani ya ATEC II na CPA (T) pamoja na wale wa CPA (T) Equivalent wanatakiwa kuwasilisha picha zao kwa ajili ya kutengenezewa vyeti kabla ya Januari 30, 2020. Tangazo juu ya namna ya kuwasilisha picha hizo liko kwenye tovuti ya Bodi," alisema.
BOFYA HAPA KUYATAZAMA MATOKEO HAYO
BOFYA HAPA KUYATAZAMA MATOKEO HAYO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...