KWA zaidi ya Muongo mmoja sasa, Mitandao ya kijamii imetumika kama njia ya mawasiliano kwa marafiki zetu tuliopotezana siku nyingi mitandao imekuwa zana ya kupata taarifa iwe  kuhusu biashara, jabari, masoko hata utani; watu ulimwenguni pote wanatumia mitandao ya kijamii kwa madhumuni mbalimbali na  kupatikana kwake ni rahisi kuliko hapo nyuma, na kuna nchi na baadhi ya maeneo imefikiwa zaidi na mitandao kuliko kwingine. 

Takwimu zinaonyesha kwamba, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa ni njia bora ya Kidigitali ya masoko ya Kimataifa na hiyo ni kutokana na namna inavyoweza kutangaza na kukuza masoko ndani na nje ya nchi pamoja na uteuzi wa mtandao upi ambao utafikisha taarifa kwa haraka na kuleta matokeo chanya.

Ni nchi gani zinatumia zaidi mitandao ya Kijamii? 

Umewahi kujiuliza au kudadisi kuwa ni nchi ipi ni kinara wa mitandao ya kijamii?  Ufilipino ndio nchi yenye watu wanaotumia zaidi mitandao ya kijamii. Mpaka kufikia mwaka 2018, Ripoti ya Masuala ya Digitali ya Ulimwengu(Global Digital Report) iliitaja Ufilipino kama mtumizi mkuu wa mitandao ya kijamii. Ni kwa miaka miwili, Ufilipino imebaki kuwa kinara. 

Watumiaji wa Mitandao huko Ufilipino wanatumia wastani wa saa 3 na dakika 57 kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Hii ni theluthi moja tu ya muda ambao wanatumia inteneti kila siku (Saa9 na dakika 29) na kuifanya Ufilipino kuwa nchi ya pili kwa matumizi ya inteneti baada ya Thailand.

Wakazi milioni 67 nchini humo wanatumia mtandao wa Facebook sambamba na wengine milioni 10 wanaotumia Instagram. Asilimia 10% ya watumiaji wa Mitandao ya kijamii pia ni watumiaji wa YouTube ndani ya Taifa hilo.

Kwa ujumla, Bara la Asia lina watumizi wengi wa mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa. 

Kwa ufupi huu ndio muda watu hutumia mitandao ya kijamii kulingana na Ripoti ya Masuala ya Digitali ya Ulimwengu(Global Digital Report) 2018

Indonesia – Saa 3 na dakika 23, hii ni nchi ya tatu ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii. 

Thailand – Saa 3 na dakika 10, inashika namba 4 ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii.  

Malaysia – Saa 3 kila siku, inatajwa kuwa nambari 8 Ulimwenguni

Umoja wa Falme za Kiarabu, Emerati- saa 2 na dakika 56 ikishika namba 9 ulimwenguni. 

Mitandao ya Kijamii imeendelea kutumika zaidi barani Asia hasa Saudi Arabia, ambayo imeonesha maendeleo makubwa, kati ya Januari 2017 na 2018, Matumizi ya mitandao yaliongezeka kwa asilimia 32, asilimia moja zaidi mbele ya India. Indonesia ikiwa na asilimia 23 na Vietnam 20.  

Vipi kuhusu Marekani na Canada?

Ungetarajia kuwa Marekani ingekuwa juu zaidi katika matumizi ya mitandao kwa kuwa ndipo mitandao hii inapozaliwa, Sivyo? Ushahidi unaonyesha kwamba, Marekani haikaribii hata kidogo takwimu za matumizi ya inteneti na mitandao kama ilivyo kwa Asia.  
Marekani ni nchi ya 24 kwa wastani wa matumizi ya saa 2 na dakika 1 tu kwa siku, wakati huo huo, Canada ipo nafasi ya 30 Ulimwenguni kwa wastani wa saa 1 na dakika 48 na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Global Digital Report ya 2018 iliyoeleza kwamba nchi zote mbili hazina idadi kubwa ya watumiaji wapya. Januari 2017 na Januari 2018, kulikuwa na watumiaji wapya kwa asilimia 9 nchini Canada na asilimia 7 nchini Marekani. 

Kwa kuwa mitandao ya kijamii ilianza kuwa maarufu Marekani na intaneti yenye kasi zaidi, inafanya uwekaji wa vitu mitandaoni kuwa wa haraka na na hivyo muda mchache kutumika kulinganisha na maeneo mengine. 

Kulingana na kituo cha Utafiti cha Pew, Mitandao ya Kijamii imekuwa ni muunganiko wa tabia zinazoibuka na zile za umaarufu ambazo zimekuwepo kwa kipindi kirefu ndani ya Marekani. Facebook na YouTube zinatumika zaidi, angalau  73% ya watu wazima wote hupachika maandiko kwenye Facebook, na 68% kutazama video kwenye YouTube. Vijana wengi kati ya umri wa miaka 18 had 24, wanatumia Snapchat kwa 78%, na 71% huingia mara tatu kwenye mtandao huo kila siku. Pia kuna 71% ya vijana ambao hutafuta au kupakia picha kwenye mtandao wa Instagram, 29% hutumia Pinterest na karibu 25% hutumia mtandao wa kibiashara na kazi wa LinkedIn.


Huko Canada, Facebook imekuwa mtawala zaidi kuliko hata ilivyo Marekani. Mamlaka ya Uthibiti ya Canada (Canadian Internet Registration Authority-CIRA) inaeleza kwamba 77% ya wakanada wote wapo Facebook. Lakini baada ya Facebook raia wa Canada wanapendelea mitandao ya Instagram na LinkedIn (35%), kisha mtandao wa Twitter (26%), na Snapchat (19%). Canada ni namba tatu kwa umaarufu wa shughuli za mitandaoni, na kuifanya mtumizi mkubwa wa Inteneti karibu 67%. 

Kupokelewa kwa Mitandao ya Kijamii

Ukitazama ulinganifu wa matumizi ya mitandao ya kijamii, utajiri wa Taifa Fulani sio kigezo kabisa, Unaweza kufikiri nchi tajiri ndio itakuwa na watumiaji wakubwa wa mitandao. Sivyo, na sio lazima iwe hivyo. 

Nchi za Mashariki ya Kati zina sifa ya uchumi ambao unaendelea, Lakini Ukanda huo una matumizi makubwa ya Mitandao ya Kijamii kuliko pengine popote. Pew Research Center inaeleza kwamba 75% ya watu wa Jordan wanatumia mitandao ya kijamii, Lebanon ni 72%.

Nchi zenye uchumi imara zina matumizi madogo ya mitandao ya kijamii, mfano Ujerumani ni 40% na Japani ni 39%. Hii ni chini wa Wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii ulimwenguni ambayo ni 53%.

Uingereza pia watu wanatumia muda mchache kati katika mitandao ya kijamii kulinganisha na Marekani ingawa 85% ya watu wote wanatumia mitandao. 

Ripoti za hivi karibuni zinaonesha kwamba Facebook, Facebook Messenger, WhatsApp, na Instagram inatumiwa sana Uingereza ingawa Facebook inatumika zaidi lakini Instagram na WhatsApp zimejikusanyia watumiaji wengi miaka ya karibuni. 

Jambo lingine muhimu ni kwamba, katika nchi zilizoendelea, Wanawake wanatumia zaidi Mitandao kuliko wanaume. Mfano Sweden, Wanawake wanaotumia mitandao ni 72% ukilinganisha na Wanaume ambao ni 63%. Ingawa Wanaume wanatumia zaidi intaneti kwa 94% huku wanawake ni 90%

Kwa nini Mataifa yanatumia Mitandao ya Kijamii? 

Sababu kubwa ya Ufilipino kuwa na matumizi makubwa ya Mitandao ni idadi kubwa ya watumiaji wanaopakia maandiko kila kukicha lakini pia idadi kubwa ya watu wanaoitembelea nchi hiyo. 

Huko Ulaya, Wengi hupata habari kupitia mitandao mfano tu, Nchini Italia, Nusu ya Raia wote wanatumia mitandao kupata Habari.  Angalau 40% ya watu wanapata habari kupitia mitandao katika nchi hizi Uhispania, Denmark, na Sweden. Facebook ndio inatumika zaidi kupata Habari mbalimbali.

Ikiwa na mionekano mipya na ya kuvutia, Wafanyabiashara wengi sasa wanaitumia Mitandao kuwasiliana na wateja wao. Nchi kadhaa zinatumia Mitandao kwa biashara. Ingawa sababu za matumizi ya mitandao zinatofautiana kulingana na watumiaji, ukubwa wa matumizi na mengineyo lakini ukweli ni Kwamba mitandao imekuwa na thamani kubwa sana wakati huu kuliko kipindi chochote kihistoria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...