Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua darasa katika Shule ya Msingi Ng’ao, iliyopo wilayani Ruangwa,
wakati akikagua miradi ya Halmashauri, Desemba 31, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua vitanda katika Shule ya Lucas Maria, iliyopo wilayani Ruangwa,
wakati akikagua miradi ya Halmashauri, Desemba 31, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua maabara katika Shule ya Lucas Maria, iliyopo wilayani Ruangwa,
wakati akikagua miradi ya Halmashauri, Desemba 31, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiuliza jambo kwa Mshauri wa Mradi Sudi Shomari, wakati alipotembelea
mradi majengo ya VETA, yanayojengwa katika Kata ya Nandagala wilayani
Ruangwa, wakati akikagua miradi ya Halmashauri, Desemba 31, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua mradi wa majengo ya VETA, yanayojengwa katika Kata ya Nandagala
wilayani Ruangwa, wakati alipotembelea miradi ya Halmashauri, Desemba
31, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua maabara ya hospitali mpya ya Wilaya ya Ruangwa, wakati
alipokagua miradi ya Halmashauri, Desemba 31, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akifafanuliwa jambo, baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, wakati alipokagua miradi ya
Halmashauri hiyo, Desemba 31, 2019. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………
*Kama kuna wahusika walioko likizo warudishwe haraka
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya shule
ikamilike mapema na kama kuna watendaji walioko likizo warudi kwani
Serikali inataka wanafunzi wote waanze masomo pamoja.
Ameyasema
hayo leo (Jumanne, Desemba 31, 2019) wakati alipofanya ziara kukagua
ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleoa wilayani Ruangwa. Amesisitiza
ukamilishwaji wa miradi hiyo ili wananchi waanze kuitumia.
Waziri Mkuu
amesema agizo alilolitoa kwa wakuu wa mikoa Desemba 29, 2019 kuhusu
usimamizi wa miundimbinu ya shule ikiwemo ujenzi wa madarasa liko pale
pale kwa sababu Serikali haitaki kuona wanafunzi wakipishana katika
kuanza masomo.
Miradi ambayo
Waziri Mkuu ameitembelea ni ujenzi wa shule ya msingi ya Ng’au ambayo
ipo katika hatua za mwisho kukamilika, ujenzi wa chuo cha VETA,
hospitali ya wilaya ya Ruangwa na shule ya sekondari ya Lucas Maria.
Waziri Mkuu
amesema Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya
maendeleo hivyo ni lazima viongozi katika maeneo husika wahakikishe
wanashirikiana katika kusimamia utekelezaji wake.
Amesema
wanafunzi wanatakiwa kuanza masomo mwanzoni mwa mwezi Januari, 2020,
hivyo ni lazima usimamizi ukaongezwa katika baadhi ya maeneo ambayo
miundombinu yake bado haijakamilika ili kuwahi masomo.
Akiwa katika
shule ya Sekondari ya Lucas Maria Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue ahakikishe
mafundi wanafanya kazi usiku na mchana.
“Shule
zinakaribia kufunguliwa na baadhi ya majengo kama bwalo, maabara, nyumba
za walimu hayajakamilika mafundi hawapo eneo la ujenzi na Serikali
imetoa fedha. Nataka kazi hii ikamilike mapema kwani hakuna sababu.”
Wakati huo
huo, Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wamepongeza na kumshukuru Rais wa
Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na miradi ya kimkakati
inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Wananchi hao
wakiwemo vijana wanaojenga chuo cha VETA walitoa pongezi na shukrani
hizo mbele ya Waziri Mkuu baada ya kumaliza kukagua mradi wa ujenzi wa
chuo hicho. Mafunzo yatakayotolewa chuoni hapo ni pamoja na ufundi
uashi, seremala, magari, ushonaji nguo na Tehama.
Kadhalika,
vijana hao wamewashauri vijana wenzao wajitokeze na kuchangamkia fursa
za ajira zinazopatikana katika maeneo yao kupitia miradi mbalimbali
inayotokelezwa na Serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...