Mtumishi
mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kitengo cha
ugawaji dawa anayejulikana kwa jina la Francis Mlesa (33) anashikiliwa
na Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa tuhuma ya wizi wa a dawa zikiwemo
za ARVs
Akizungumza na blog hii
Ofisini kwake Ofisa Tarafa ya Igunga mjini Shadrack Kalekayo amesema
tukio hilo lilitokea disemba 24 mwaka huu ambapo mtumishi huyo
alishitukiwa na mlinzi aliyekuwa zamu majira ya sasa Mona na nusu usiku
baada ya kumuona amefunga maboksi mawili kwenye baiskeli
Kalekayo
amesema baada ya kukagua maboksi hayo ilibainika kuwa zilikuwemo dawa
aina ya ARVs ila mtumishi huyo alifanikiwa kutoroka nazo baada ya mlinzi
kuzidiwa na watu wanaopita getini hapo
Mlinzi
aliyekuwa zamu siku hiyo Rushina ngeme Paulo alithibitisha kumkamata
mtumishi huyo na dawa hizo akidai kuwa zimeisha muda wake na akidai kuwa
alikuwa anaenda kuziteketeza ila mlinzi huyo alipoziangalia aliona kuwa
zilikuwa hazijaisha muda wake
Amesema
kuwa alitoa taarifa kwa uongozi wa Hospitali hiyo disemba 26,2019 na
alifikishwa mbele ya uongozi ambapo alikiri kuiba dawa hizo huku akisema
alizichukuwa kwa ajili ya kuziteketeza moto
Kwa
upande wa watumishi wa Idara ya Afya hospitalini hapo ambao hawajataka
majina yao yajulikane wamesema mtumishi huyo amekuwa akiwauzia
Wafanyabiashara wa Ng'ombe kwa ajili ya kunenepesha mifugo yao
Kwa
upande wake kamanda wa TAKUKURU Wilayani hapo Fransis Zuakuu
amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku akisema alipigiwa simu na raia
wema wakimjulisha kuwa kuna mtumishi ameiba dawa hospitalini na kutoroka
nazo ambapo baada ya kumtafuta na kumkosa alimwagiza Mganga mkuu wa
Wilaya hiyo Deus Ruha kumsaka ambapo disemba 26 walimpata na tayari yupo
mahabusu katika kituo cha polisi Wilayani hapo
Aidha
Nzuakuu ametoa wito kwa watumishi wa idara zote kufanya kazi kwa
uadilifu na kujiepusha na vitendo kama hivyo kwani Serikali haitafumbia
macho mtumishi Yeyote atakayebainika na vitendo kama hivyo vya wizi wa
dawa za Serikali
Hata
hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora ACP Barnabas Mwakalukwa
alipoulizwa juu ya tukio hilo amethibitisha kushikiliwa kwa Francis
Malesa huku akisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala lolote kwani bado
wanaendelea kumhoji ili kubaini thamani ya dawa zilizoibwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...