Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa Kibaha Crossman Makere wakielekea yalipo mabomba ya DAWASA yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuleta maji katika kiwanda cha TanChoice kilichopo katika wilaya ya Kibaha mkoni Pwani.
Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa Kibaha Crossman Makere akitoa ufafanuzi kuhusu mambomba yaliyowekwa kwenye Kiwanda cha Kiwanda cha nyama  cha TanChoice kwa ajili ya kuunganishiwa maji kutoka DAWASA. Wa Julia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  na Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Juma.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kibaha, DAWASA pamoja na viongozi wa kiwanda cha TanChoice mara baada ya kufanya ziara hapo ili kujionea uwekaji wa mabomba ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
 Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) yaliyopo katika kiwanda cha TanChoice wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji katika wilaya Kibaha mkoani Pwani
 Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  akitoa maelekezo kwa viongozi wa DAWASA pamoja na RUWASA mara baada ya kuleta mradi wa maji kwenye kijiji cha Kipangege uliokwamishwa na utendaji mbaya wa viongozi wa RUWASA wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
 Wananchi wa Kipangege wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  wakati akitafuta ufumbuzi wa upatikanaji wa maji katika kijiji hicho mara baada ya mradi huo kutumia miaka sita bila kukamilika ulikuwa unasimamiwa na RUWASA.
  Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Makazi Mapya wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji iliyo chini ya wizara yake katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Eng.Ramadhani Mketo akitoa taarifa fupi ya namna ya wananchi wa Kitongoji cha Makazi mapya kata Kawawa wilaya ya Kibaha watakavyonufaika na mradi wa maji ya DAWASA kwa njia ya mabomba kwa kila mkazi wa eneo hilo ambapo sasa wanatumia maji ya Kisima ya DAWASA.
 Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Juma akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Makazi mapya kata Kawawa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  ya ukaguzi wa miradi ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na RUWASA. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kulia ni Diwani wa kata ya Kawawa Salum Salum Lubawa.
 Diwani wa kata ya Kawawa Salum Salum Lubawa akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) waliofika katika  Kitongoji cha Makazi Mapya ili kuweza kutatua kero ya maji katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Makazi Mapya kata Kawawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Maji iliyopo katika wilaya Kibaha mkoani Pwani.

 NAIBU WAZIRI wa maji Juma Aweso amewataka wataalamu wa maji Kibaha Mkoani Pwani kutoa huduma ya maji kwa uhakika sio kusubiri Hadi viongozi waje Ila wafanye kazi hiyo ukiwa ni sehemu ya wajibu wao katika kutekeleza miradi ya maji.

Amesema kuwa mradi wa maji wa Kipangege ambao hadi Sasa  jumla ya shilingi milioni 151 zimetolewa na mkandarasi kulipwa shilingi 125 lakini mradi huo una miaka 6 na utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana baadhi ya wafanyakazi wa RUWASA kuhujumu mradi huo.

Amesema kuwa kuna baadhi ya  viongozi wamekuwa sehemu ya kuhujumu Serikali hivyo ni vyema wakajitathimini kwa kuwa Serikali ina mkono mrefu na haitamfumbia macho yeyote atakayebainika anafanya hujuma hizo.

"Tumefika hapa tumesikia Mkurugenzi wa mradi wa RUWASA amempigia simu mkandarasi akimbie, hatutavumilia viongozi yeyote atakayehujumu serikali kwa namna yoyote ile" ameeleza.

Amesema waliohusika kuhujumu mradi huo watachukuliwa hatua Kali za kisheria na amewataka wasimamizi wa miradi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwasaidia wananchi.

Kwa upande wake meneja wa DAWASA Mkoa wa kibaha Crossman Makere amesema licha ya Waziri kutembelea miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kiwanda cha nyama maagizo yaliyotolewa ikiwemo kutekeleza miradi yote ifikikapo Januari watazingatia kwa kuwa vifaa vyote vipo site na huduma za maji katika Mikoa yote itafika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Assumpter Mshama amesema kuwa utekelezaji wa miradi  maji unahitaji usimamizi mkubwa kutokana na umuhimu wa huduma hiyo.

Amesema kuwa Wilaya ya Kibaha hasa vijijini Kuna changamoto kubwa ya maji na kuiomba Serikali kuliangalia hilo kwani limeleta migogoro iliyopelekea kifo kutokana na ukosekanaji wa huduma ya maji.

Amesema kuwa wamekuwa wakivuna maji ya mvua ili kupambana na ukosefu wa maji, na kueleza kuwa wasimamizi wa miradi hiyo wanasaidia Serikali katika kuhakikisha huduma hizo za msingi zinafika kila eneo hasa vijijini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...