Meneja Ukuzaji wa Biashara wa NBC, Jonathan Bitababaje akichangia mada wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao jijini Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kwa makini baadhi ya mada zilizokuwa zikitolewa katika Semina hiyo kutoka wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Mapato (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (Brela), Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na wengineo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakisikiliza baadhi ya watoa mada katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wafanyabiashara hao juzi.
Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), George Chuwa akizungumza wakati semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kulia) akisalimiana na
wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo katika semina ya
siku moja ilyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo
kuhusu ukuaji za mbinu za kufanya biashara zao jijini Dar es Salaam
jana.
Meneja
wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (kulia),
akizungumza na wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini humo jana
kuhusu huduma na bidhaa zotolewazo na benki hiyo hususani wakati wa
semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na wadau muhimu
kutoka taasisi mbalimbali zinazuhusika na masuala ya biashara.
Mwakilishi
kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Gwakisa
Bapala (kulia), akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na baraza
hilo wakati wa semina kuhusu mbinu mbalimbali za kufanya biashara
iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati
katika Ukumbi wa Hoteli ya Millenium Towers jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu
wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance
Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja ya wafanyabiashara
wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo iliyoandaliwa na benki hiyo kwa
lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao jijini
Dar es Salaam juzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...