Watumiaji wa pombe kali zinazosambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wana kila sababu ya kufurahi msimu huu wa sikukuu, baada ya kutangazwa kwa punguzo kubwa la bei kwa aina mbali mbali ya vinywaji vikali.
Ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuwajali katika msimu wa sikukuu, SBL jana ilizindua punguzo kubwa la bei kwa vinywaji vyake vikali ili kuwawezesha wateja wake kuwanunulia ndugu jamaa na marafikizawadi za vinywaji vyenye ubora wa kimataifa kwenye sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.
Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wake kufurahia sikukuu pamoja na wawapendao kwa kuwanunulia pombe kali zinazosambazwa na kampuni hiyo kama Johnnie Walker, Captain Morgan, Ciroc, Smirnoff Vodka na nyinginezo kwa punguzo kubwa la bei.
“Kampeni hii ya kutoa zawadi, inaenda sambamba na wito wetu wa kunywa kistarabu ambapo tunawaelimisha wateja wetu kuepuka kutumia vilevi na kisha kuendesha vyombo vya moto,” alisema Ocitti.
Ni mwaka wa tano sasa kampuni ya SBL inaendesha ya kampeni ya unywaji wa kistarabu kwa kushirikianba na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani.
Kwa upande mwinginre, Ocitti alizungumzia mwenendo wa kibiasahara wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanda vyake vya Dar es Salaam na Moshi unaogharimu Pauni za Uingereza milioni 14. Upanuzi huo utakapokamilika, utaiongezea kampuni hiyo uwezo wa uzalishaji kwa asilimia 34 zaidi.
“Upanuzi tunaofanya, unaonyesha nia yetu ya kupanuka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zetu pamoja na kutengeneza ajira zaidi. Upanuzi huu pia utaongeza mahitaji ya malighafi tunazonunua kutoka kwa wakulima wa ndani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu,” aliongeza.
Kampuni ya SBL imenunua tani 17,000 za ujazo za mahindi na uwele kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya jumla ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka. SBL pia imelipa jumla ya shilingi 121bn/- kama kodi za aina mbali mbali kwa mujimu wa Ocitti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.
Meneja Afya na Usalama Mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) David Mwakalobo (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...