Charles James, Michuzi TV

UMESIKIA walichokutana nacho Hugo Lloris, Harry Kane? Iko hivi Tottenham Hotspur waliendesha zoezi la kuwapata wachezaji wao bora kwa nafasi mbalimbali kwa kipindi cha muongo mmoja (miaka 10).

Sasa katika eneo la golikipa nafasi hiyo ilikua ikishindaniwa na Gomes, Brad Friedel na Hugo Lloris. Sass kwa kuwa Friedel aliwahi kucheza Liverpool mwaka 1997-2000 basi mashabiki wa Liverpool wakaingilia box la kura huko Twitter matokeo yake Friedel akashinda.

Ubabe ulikua kwenye tuzo ya mshambuliaji bora ambapo ilikua ikiwaniwa na Jermaine Defoe, Harry Kane na Peter Crouch.

Mwanzo Kane alikua akiongoza kwa asilimia 90 lakini Liverpool walivyoweka post hiyo Twitter upepo ukabadilika Crouch ambaye alipita Anfield mwaka 2005-2008 akashinda na kuwa mshambuliaji bora wa Spurs licha ya Crouch mwenyewe kumuombea kura Kane.

UKUMBUSHO: Misimu miwili nyuma Liverpool walihamasishana kumpigia kura Lucas Leiva kuwa mchezaji bora wa Lazio. Kumbuka Leiva aliwahi kucheza Liverpool.

Yaani wasije wakajichanganya tuzo ya mchezaji bora wa Dunia iwe inapigiwa kura online na mshindi apatikane kwa kura za mashabiki online Liverpool itashinda kila mwaka.
 Kiungo wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anakipiga kunako Klabu ya Lazio ya Italia, Lucas Leiva.
 Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Tottenham Hotspur na Timu ya Taifa ya England, Peter Crouch akiwa na jezi ya Liverpool ambayo aliitumikia kwa misimu mitatu kuanzia 2005-2008
Golikipa wa zamani wa Liverpool na Tottenham Hotspur, Brad Friedel akiwa kwenye majukumu yake na jezi ya Spurs. Friedel jana ameshinda tuzo ya kipa bora wa Spurs kwa kipindi cha muongo ulipita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...