Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Masuala ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (wa
pili kutoka kulia) akizungumza na Wadua walioshiriki katika Mkutano
kuhusu masuala ya Utoaji wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu uliofanyika
katika Hoteli ya Nashera, Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wadau walioshiriki
Mkutano huo wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Masuala ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (hayupo
pichani).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama
vya Watu Wenye Ulemavu Taifa (SHIVYAWATA) Bw. Jonas Lubago akielezea
jambo wakati wa Mkutao huo uliowakutanisha wadau kujadili kuhusu
umarishwaji wa masuala ya Utoaji wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu. Wa
tatu kutoka kulia Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Masuala ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa.
Mtaalamu Mwelekezi kutoka Chuo Cha
Mzumbe Dkt. Henry Mollel (aliyesimama) kiwasilisha mada kuhusu rasimu
ya mpango huo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye Mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha
Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu Bw. Philbert Kawemama (kulia) akifafanua
jambo wakati wa Mkutano huo. Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulika Masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.
Stella Ikupa, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu Wenye
Ulemavu, Dkt. Lucas Kija na Afisa Programu kutoka Shirika la Foundation
for Civil Society, Bi. Eveline Mchau.
Mwakilishi kutoka Chama cha Wasioona Bi. Nuru Awadhi akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulika Masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau walioshiriki
Mkutano kuhusu masuala ya Utoaji wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu
uliofanyika katika Hoteli ya Nashera, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.
Stella Ikupa (kushoto) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Ushauri kwa Watu Wenye Ulemavu, Dkt. Lucas Kija (mwenye tai) baada
ya Mkutano masuala ya Utoaji wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu
uliofanyika. Wa kwanza Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya
Watu Wenye Ulemavu Taifa (SHIVYAWATA) Bw. Jonas Lubago, Bi. Josephine
Liyengi. Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha
Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu Bw. Philbert Kawemama.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Serikali
imedhamiria kuandaa Mpango wa Taifa wa kuimarisha masuala ya utoaji
huduma kwa Watu wenye Ulemavu ili kuwezesha kundi hilo maalumu kushiriki
kwenye sekta mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Watu
wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa alipokuwa akifungua mkutano wa wadau
kuhusu masuala ya utoaji huduma kwa Watu wenye Ulemavu uliofanyika
Disemba 11, 2019, Jijini Dodoma.
Akizungumza
wakati wa Mkutano huo Naibu Waziri Ikupa alieleza kuwa lengo la Serikali
kuandaa mpango huo ni mkakati mmoja wapo wa kuwezesha Watu wenye
Ulemavu wanapata huduma bora ikiwemo elimu bora, afya, fursa ya kufanya
maamuzi mbalimbali pamoja na kuwezeshwa kiuchumi.
“Utekelezaji wa
Mpango huu utakuwa wa miaka mitano na Rasimu ya mpango huo imeshandaliwa
na utakapo kamilika utasaidia kwa kiasi upatikanaji wa huduma bora na
endelevu kwa Watu Wenye Ulemavu sambamba na kuimarika kwa utekelezaji wa
Sera, Sheria, Miongozo pamoja na Mifumo mbalimbali ya Usimamizi wa
kundi hilo maalum,” alisema Ikupa
Aliongeza kuwa
mpango huo unalenga pia kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika
kushughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, kuboresha utoaji huduma,
kuimarisha shughuli za kiuchumi na ajira, upatikanaji wa taarifa na
takwimu muhimu za watu wenye ulemavu, na pia ushiriki na ushirikishwaji
wa watu wenye Ulemavu.
“Ninaamini maoni
mbalimbali ya wadau yakayotolewa katika mkutano huu yatasaidia kwa kiasi
kikubwa uimarishwaji wa mpango huo wa taifa wa utoaji huduma kwa watu
wenye ulemavu,” alisema Ikupa
Sambamba na hayo,
alielezea pia mkutano huo utatoa fursa kwa wadau kutoa maoni yao juu ya
mwongozo wa usimamizi, uratibu na uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Watu
wenye Ulemavu ulioanzishwa kwa Sheria Na.9 ya mwaka 2010.
“Uwepo wa Mfuko
huo utawezesha Watu wenye Ulemavu kukuwa kiuchumi na utawajengea uwezo
wa kujiamini na kuanzisha miradi na shughuli mbalimbali zitakazowakwamua
kiuchumi,” alieleza Ikupa
Aidha, Naibu
Waziri Ikupa alitoa wito kwa wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi na
kuchangia mfuko huo ili kufanikisha lengo la kuimarisha maisha na huduma
za watu wenye ulemavu, na pia alihimiza vyombo vya habari kutangaza
mfuko huo.
Kwa upande Wake,
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu Wenye Ulemavu, Dkt.
Lucas Kija alieleza kuwa Watu wenye Ulemavu wamekuwa wakikabiliana na
changamoto ambapo imepelekea wamekuwa wakikosa haki zao na huduma
stahiki.
“Mpango huu wa
Serikali utatoa mwongozo wa kuhudumia masuala ya watu wenye ulemavu
katika sekta ya elimu, afya, ajira, uwezeshaji kiuchumi, miundombinu ili
kuleta ustawi wa kundi hilo maalumu, hivyo mpango huo utaifanya jamii
kuthamini Watu wenye Ulemavu,” alisema Lubago
Naye Afisa
Programu kutoka Shirika la Foundation for Civil Society, Bi. Eveline
Mchau alisema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ili
kufanikisha masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...