Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akiwahahihishia na
wafanyabiashara wa Sanaa ya ufundi na wachongaji wa vinyago wanaofanya
shughuli zao katika kijiji cha mwenge vinyago leo jijini Dar es Salaam
kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro wa eneo hilo ndani ya mwaka
2020 alipotembelea eneo hilo kwa ajili kuwataka kuacha kutofautiana
kwani hilo ndiyo linalokwamisha kumalizika kwa mgogoro huo.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto)
akitembelea mabanda ya wafanyabiashara wa sanaa za ufundi wanaoendesha
shughuli zao katika kijiji cha mwenge vinyago katika ziara yake ya
kikazi katika eneo hilo,(wa kwanza kulia) Katibu Mkuu wa Chama cha
wachonga vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Bibi.Joyce Fisoo akiwahakikishia ushirikiano kutoka wizarani wachongaji
wa vinyago na wafanyabiashara wa sanaa ya ufundi wanaoendesha shughuli
zako katika eneo la kijiji cha mwenge vinyago alipowatembele jana katika
eneo hilo jijini Dar es Salaam,(wa kwanza kulia) Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi.

Rais wa Shirikisho la Sanaa za
Ufundi Tanzania Bw.Adrian Nyangamale akiomba viongozi wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa tamko la kulitaka Baraza la
Sanaa la Taifa kutoa mwongozo wa kusimamima uendeshaji wa shughuli
mbalimbali katika eneo Kijiji cha Mwenge vinyago Jijini Dare s
Salaam,walipotembelewa na viongozi wa Wizara hiyo,(wapili kulia) Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally
Possi.

Baadhi ya wasanii wa kuchonga
vinyago na wafanyabiashara wa sanaa ya ufundi wanaoendesha shughuli zao
katika eneo mwenge vinyago wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi
(aliyeketi wanne kutoka kulia)mara baada ya kikao na wadau hao katika
eneo hilo,(watatu kushoto) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa
kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo na
(wakwanza kulia aliyeketi) Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi
Tanzania Bw.Adrian Nyangamale.
……………..
Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amewahikikishia
wasanii wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mwenge Vinyago kuwa
serikali itahakikisha inamaliza mgogoro wa eneo hilo ndani ya mwaka
2020.
Dkt.Possi ametoa kauli hiyo leo
Jijini Dar es Salaam alipotembelea eneo hilo la wachogaji wa vinyago na
wauzaji wa kazi za sanaa za ufundi lilopo Mtaa wa Nzasa kata ya mwenge
kwa lengo la kufahamu ukubwa wa eneo hilo pamoja na kuzungumza na wadau
wanaoendesha shughuli zao eneo hilo na kufahamu changamoto zao.
“Eneo hili ni kubwa na nieneo la
kimkakati kabisa kuendesha biashara zenu hivyo serikali imedhamiria
inatatua kero yenu ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi hii uliyodumu kwa
miaka mingi kwani ili kila mmoja wenu aweze kuendesha shughuli zake za
kujipatia kipato na hata atakapopatikana mwekezaji basi aweze kuwa huru
kuwekeza na kuboresha miundombinu ,“alisema Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza katika kikao
hicho na wadau hao Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwasahii wadao hao kuacha
kuwa na makundi na kutofautiana kwani migogoro hiyo ndiyo
itakayokwamisha kukamilika kwa kutatuliwakwa kero za eno hilo hivyo wawe
wamoja na waache kumfuatisha huyo anayewajengea chuki miongoni mwao na
kuleta mgawanyiko.
Aidha, nae Katibu wa Chama cha
Wachogaji wa Vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani alitoa ombi la
mazingira ya eneo hilo kuboreshwa katika suala la ulinzi,usafi kwani
itasadia wasanii wachongaji wanaofanya shughuli zao kuzifanya kwa
ufanisi zaidi na kuongeza ubunifu ambao utalitangaza taifa vyema.
“Ukosefu kwa mafunzo stadi za
sanaa ya uchongaji wa na uhaba wa vitendea kazi vya kisasa umekuwa ni
kero ya inayokwamisha maendeleo ya kazi hii,”alisema Bw.Ramadhani.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo wa
CHAMUSATA alitoa maombi ya kwa BASATA kutoa tamko juu ya mwongozo wa
matumizi ya eneo hilo sababu ndiyo waliyokabidhiwa kusimamia eneo hilo
kwa tamko la Mheshimiwa Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe tangu mwaka 2018.
Halikadhalika kwa upande wa
Mhasibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Onesmo Kayanda
aliyemuwakilisha Katibu Mtendaji wa Baraza hilo aliahidi kupokea
maelekezo yote yaliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu huyo maara baada ya
risala ya chama cha wachongaji vinyago Tanzania kusomwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...