Mkurugenzi wa huduma za Elimu -CSSC Mwl.Petro Pamba ,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoriki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] uliofanyika leo jijini Dodoma.
Na.Charles James, Michuzi TV
kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala kutoka Tamisemi Dkt. George Jidamva ametoa Rai kwa Taasisi za dini za Elimu hapa nchini kuhakikisha zinaitumia vyema Tume(cssc), ili liwe Daraja imara la kuwasilisha hoja serikalini.
Dkt.Jidamva ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipomuwakilisha Naibu katibu mkuu Elimu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Bw.Gerald Mweli, amesema Tume ya kikristo ya huduma za jamii[CSSC] imekuwa na Mchango mkubwa katika jamii hivyo ni vyema ikaungwa mkono kwa jitihada zote za kusimamia ubora wa elimu nchini kwa makanisa
“Ni jambo jema kwamba wazazi wengi wanafurahishwa na juhudi za Makanisa katika utoaji wa elimu nchini,ni imani yangu mtaendelea kutoa elimu iliyobora na Maadili mema kwa kufuata taratibu,sera,sheria na miongozo iliyopo hivyo tume ya CSSC imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi, na nitoe rai tu kwa Taasisi za Makanisa kuitumia vyema ili liwe daraja imara la kuwasilisha hoja kwa serikali”amesema.
Aidha ,ametumia Fursa hiyo kuipongeza TUME ya kikristo ya huduma za jamii( CSSC ) kwa kuanzisha Huduma ya udhibiti ubora ,uhakiki wa Takwimu na Mitihani ya pamoja kwa Madarasa ya Mitihani kitaifa huku akiasa kuweka Mazingira Mazuri ya Ushirikiano kwa ngazi ya kata na Halmashauri.
Hata hivyo ameshauri ombi la asilimia moja ya gharama za uendeshaji wa shule [WCF] kufanana na ya serikali ya asilimia 0.5 iletwa kwa maandishi yenye ufafanuzi na Tume kwa hatua zaidi.
Mkurugenzi wa Elimu wa Tume Kikristo ya Huduma za jamii[CSSC]Mwalimu Petro Masatu Pamba amesema ufaulu kwa shule za makanisa umekuwa chachu nchini ambapo mwaka 2013 hadi 2018 matokeo ya kidato cha nne kwa shule zilizo na wanafunzi zaidi ya 40 ,shule 100 bora ,kanisa limekuwa na ufaulu wa wastani wa asilimia 70%.
Pia amesema Makanisa yameendelea kuboresha ufundishaji wa Masomo ya sayansi kwa kutumia TEHAMA.
“shule 42 mpaka sasa zinatumia mfumo huu kwa uratibu wa PLATFORM ya Tume Walimu,wanafunzi na Menejimenti ya Shule kuboresha umahiri kwa wanafunzi na matumizi ya utawala”amesema.
Akitoa neno la Shukrani, Padri kutoka jimbo katoriki la Moshi mkoani Kilimanjaro ,Padri.William Ruwahi’ch ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini .
”Tunashukuru sana kwa serikali kwa kuendelea kuthamini mchango wa shule za kanisa ,tunaahidi kuhakikisha tunatoa elimu bora”amesema.
Aidha,amesema kuna changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na leseni ya Biashara kwani taasisi za kanisa zinatoa huduma na si za kibiashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...