Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw.Carter ametoa shukrani zake za dhati kwa mwakilishi wa Waziri Mkuu ambaye alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama na TACAIDS katika Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza kwa kuipa TUZO Kampuni ya StarTimes na kusema kwamba itajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuchangia na kuisaidia Serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Kadhalika Startimes imepata Tuzo hiyo kupitia Jukwaa la Bongo Star Search kinachoruka ndani ya Chaneli ya ST Swahili, imelenga Kusaidia na kuelimisha vijana juu ya maambukizi ya VVU ambao vijana ndio walengwa wakubwa.
Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw.Carter Alitoa mchango wa Shilingi MillionI Tano(5,000,000/=) kuchangia mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI.
“Ni heshima kubwa sana kupokea Tuzo ya TACAIDS. Sisi Kampuni ya Star Media Tanzania tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kusaidia Serikali kwa kuchangia kupiga vita maambuki ya Virusi vya Ukimwi Tanzania na kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030.” Alisema Makamu wa Rais wa kampuni ya Star Media(StarTimes)Bw Carter
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Shilingi Millioni Tano (5,000,000/=) kutoka kwaMakamu wa Rais wa kampuni ya Star Media(StarTimes)Bw Carter kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI wakati wa maadhimisho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...