Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salumu akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa njia ya vidole Babati mkoani Manyara.
Elizabeth Kitundu Mkuu wa Wilaya ya Babati akizungumza katika mkutano huo na wananchi waliojitokeza kwaajili ya kusajili laini zao za simu pamoja na kufuata namba zao za NIDA ,Kulia kwake ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)Mhandisi Imelda Salum.
Mgeni rasmi Elizabeth Kitundu Mkuu wa Wilaya ya Babati akiwa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)Mhandisi Imelda Salumu pamoja na wadau wa mawasiliano kutoka makampuni ya simu mara baada ya kutoa elimu kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa kusajili laini zao za simu.
Emmanuel joshua-Afisa NIDA mkoa Manyara akizungumza katika mkutano huo wilaya ya Babati.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Babati wakiwa katika foleni kwenye Banda la NiDA wilayani Babati Mkoani Manyara.
Na.Vero Ignatus,Manyara
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)imeonya makampuni ya simu kuuza laini za simu bila kusajiliwa ikiwa ni mkakati wa serikali kuzuia matumizi ya laini za simu yanayokiuka maadili na sheria za nchi.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salum amesema kuwa malengo ya Serikali kusajili laini za simu ni kuhakikisha usalama wa raia unaoweza kufanyika kupitia mitandao ya simu na pale mwanamchi anapotumia huduma za mawasiliano.
Mkuu huyo wa kanda amesema kuwa mwananchi akisajili laini yake ya simu kutumia alama za vidole na kwakutumia namba za NIDA ni rahisi serikali kuwatambua watu ambao wanatumia huduma hiyo kinyume na taratibu na sheria zilivyowekwa .
Amesema kuwa mwananchi anaposajili laini yake ya simu kwa alama ya vidole na namba ya NIDA kuisaidia serikali kuwa na takwimu sahihi za watumiaji wa mawasiliano kwaajili ya mipango mbali mbali ya Serikali.
"Kuna watu wanatumia laini ishirini thelathini lakini ni laini ambazo huwezi kuzijua zinamilikiwa na nani anaweza akazitumia vibaya kuwaibia watu,kuwatapeli , kutukana wengine ,kutumia kugha za kuudhi kwenye mitandao" Alisema Mhandishi Imelda
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu ametoa wito kupitia uhamasishaji wa kusajili laini za simu wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya usajili kabla ya muda uliowekwa kufikia mwisho.
"Kifungu cha kumi cha kanuni cha kukinda watumiaji cha mwaka 2018 zinamtaka mtu yeyote anayeuza au anayetoa laini yeyote ya simu aisajili kwanza kabla haijatumika"alisema Dc Babati.
Amesema zoezi hilo linaloendeshwa na TCRA la kusajili lipo kwenye masuala ya kisheria na haitakiwi na hairuhusiwi mtu kutumia laini ya simu bila kuisajili.
Amesema kuwa TCRA kwa kushirikiana na wadau na kamati zilizoundwa ilizindua rasmi zoezi la usajili wa laini za simu kwa wa alama za vidole kwa nchi nzima ambapo usajili huo unaendelea katika maduka yote ya watoa huduma za mawasiliano pamoja na mawakala wenye vitambulisho maalum
Mhe. Kitundu amesema kuwa usajili wa majaribio ulizinduliwa rasmi machi 2018 kwenye mikoa sita ikiwemo mkoa Magharibi Zanzibar,Dar es salaam, Iringa,Singida ,Pwani na Tanga ambapo ulionyesha mafanikio makubwa.
Aidha amesema kuwa hadi sasa jumla ya laini za simu zilizosajiliwa hadi kufikia 22 Novemba 2019 jumla ya laini milioni 16.9 zimesajiliwa sawa na asilimia 38% ya laini zote za simu zinazotumika.
Mhe.Kitundu amesema Laini zote za simu zinazotumika zinakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 45 hivyo bado idadi ya waliosajili ipo chini na inaonyesha kuwa wananchi wengi haqajasajili laini zao za simu.
Serikali kupitia TCRA inarndelea kutoa elimu kwa umma juu ya usajili wa laini za simu kwa alama ya vidole na kuwahimiza watumiaji wote wa huduna za mawasiliano na kuhakikisha kuwa wanasajili laini zao kwa mujibu wa sheria za nchi.
Naye Afisa kutoka Mamlaka ya vitambulisho ya Taifa NIDA Emmanuel Joshua amesema jukumu lao kuu ni kuweza kutoa utambulisho pamoja na kutoa vitambulisho vya Taifa,ambapo wanafanya majukumu hayo sambamba,kwani kitambulisho ndicho ambacho kinatangulia ambapo kitambulisho ni matokeo ya juhudi ya kutengeneza mfumo wa utambulisho
Amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano wamekuwa wakifanya juhudi hizo kuhakikisha kuwa zoezi la usajili wa laini za simu linafanikiwa na wananchi wote wanasajili kwa kutumia alama za vidole.
Amesema kwa upande wa wilaya ya babati zoezi hilo linaendelea vizuri kwani matarajiao yalikuwa ni kusajili laini 253025 ambapo hadi sasa wameweza kusajili watu kwa asilimia 94%ya watu waliolenga kuwasajili hivyo wananchi wameitikia wito kwa wingi.
Amewataka wananchi kuweza kufuatilia namba zao za usajili kwani zoezi la kuwasajili wanachama wanachama wapya bado linaendelea,amewataka kwenda kuangalia namba namba zao katika ofisi za watendaji kwa wale ambao watakuwa wamepata changamoto waweze kufika ofisi za NIDA Manyara ili waweze kupatiwa huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...