Gati ya Bandari ya Lushamba iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiwa imekamilika baada ya Mamlaka ya Usimamizi ya Bandari nchini(TPA) kutumia Sh.bilioni 1.265 kuboresha miundombinu ya bandari hiyo ili kutoa huduma kwa wananchi wanaozunguka Visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria.
 Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kanyara Benjamin Nhungwizi akielezea faida ambazo wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria watazipata baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Lushamba iliyopo katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu katika Bandari ya Lushamba na inatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mwezi huu.Waandishi hao wapo kwenye kutembelea miradi ya TPA katika Ziwa Victoria.
 Baadhi ya waendesha  mitumbwi katika Bandari ya Lushamba wakiwa katika maandalizi ya kuanza safari ya kutoka bandarini hapo kuelekea moja ya visiwa vilivyomo katika Ziwa Victoria
 Mmoja ya wakazi wa kijiji cha Kanyara akiwa katika mtumbwi wake katika bandari ya Lushamba wilayani Sengerema ambapo ametumia nafasi hiyo kuiopongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu ya bandari hiyo
  Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza(kushoto) akiwa na baadhi ya waandishi akiangalia namna ambavyo kamera aina ya Droon ikichukua picha za bandari ya Lushamba.
 Moja ya jengo la bandari ya Lushamba likionekana kwa mbali baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya bandari hiyo



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Sengerema

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) katika Visiwa vya Ziwa Victroria imesema kuwa ujenzi wa miundombinu katika bandari ya Lushamba katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ambao umetumia Sh.bilioni 1.265 umekamilika na hivyo huduma rasmi katika bandari hiyo unatarajia kuanza mwezi huu.

Kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa bandari la Lushamba usalama wa abiria na mzigo yao hakuwa salama kwani walikuwa wakilazimika kabla kuingia kwenye chombo kuanza kupita kwenye maji hali iliyokuwa changamoto hasa kwa wagonjwa ambao hawakuwa na uwezo kabisa wa kupita ndani ya maji.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza wakati akizungumza na waandishi wa habari waliopo katika ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya uboreshaji wa miundombinu katika Ziwa hilo ikiwa ni mkakati wa TPA kuhakikisha inaboresha miundombinu ya bandari.

Amefafanua kuwa banari ya Lushamba inapatikana katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Segerema na kwamba wao kama mamlaka ya bandari wamewekeza kwa kujenga mundombinu kama inavyonekana. "Mradi huu wa ujenzi wa gati la Lushamba rasmi ulianza mwaka 2105 lakini wakati tukiwa tunaendelea na ujenzi wa upande wa gati kuna changamoto za mgogoro wa ardhi uliibuka na baada ya kuumaliza, tukaendelea na ujenzi mwaka 2018 na sasa umekamilika.

"Mradi huu kwa ujumla wake umehusisha ujenzi wa gati, jengo la abiria, jengo la kuhifadhia mizigo pamoja na eneo la vyoo na sehemu ya ulinzi. Jumla mradi hu umegharimu Sh.bilioni 1.265 kama. Matarajio ya mradi huu utaweza kutoa huduma katika visiwa zaidi ya sita ambavyo vinazunguka eneo hili la Lushamba,"amesema Mchindiuza na kuongeza visiwa hivyo vinategemea kupata huduma katika bandari hiyo ya Lushamba.

Amesema kama ambavyo ameeleza awali katika Ziwa Victoria kuna vsiwa vingi ambavyo vimejengewa miundombinu na ndani ya hivyo vsiwa kuna watu wanaishi ambao wanategemea kila kitu kisafirishwe hadi kuwafikia kwa kutegemea miundombinu hiyo ya bandari.

"Kabla ya ujenzi wa bandari hii watu moja kwa moja walikuwa wakipanda kwenye vyombo kwa kupita kwenye maji lakini pia kulikuwa na wagonjwa ambao walikuwa wanashindwa kupanda kwenye hivyo yombo vya maji.Baada ya ujenzi huu wananchi wanafurahia na wanasema sasa angalu wanao taasisi na Serikali kwa ujumla inawajali.

"Matarajio yetu ndani ya mwezi huu Bandari ya Lushamba itaanza kutoa huduma rasmi kwa kuhudumia wananchi wanaozungika visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria kwa kuanzia na kuishia hapa. Vyombo ambavyo mnaviona vimezagaa hapa kisiwani, vyote vitaanzia safari hapa kwenye gati la Lushamba , ikiwa pamoja na abiria kukata tiketi kwa ajili ya safari pamoja na kusafirisha bidhaa zao,"amesema na kuongeza ni matarajio yao kuona shehena kubwa iliyokuwa ikipita maeneo hayo sasa shehena zaidi za mizigo pamoja na abiria watapita katika bandari hiyo.

Akieleza zaidi kuhusu hali ya mazingira kabla ya ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo, Mchindiuza amesema kuwa kabla ya ujenzi wa gati hilo wananchi walikuwa wakishuka moja kwa moja kwenye maji, walikuwa wakishuhudia baadhi ya wananchi wakiangukia ndani ya maji kwa kushindwa kupanda ngazi lakini sasa mambo ni tofauti. "Kwa ujumla hali haikuwa nzuri kuumfanya mwananchi aingie kwenye chombo lakini kwa kujenga gati hili tumewasaidia kiusalama. Chombo kitapaki pembeni, abiria au mizigo itapakiwa vizuri na kisha safari kuanza".

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kanyara Benjamin Nhungwizi amesema kuwa anaishukuru Serikali kuu kwa kuliona eneo lao hilo la kwa kuweka vizuri miundombinu ya bandari na anaamini uwepo wa bandari hiyo unamanufaa makubwa kwa wananchi.

"Kwanza biashara zitaongezeka kwasababu kutakuwa na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ambao wanaoingia kuchukua biashara na wanaotoka kuchkua biashara, kwa hiyo watafaidika.Tukiangalia biashara zinazotoka visiwani sana ni samaki , zinatoka visiwani kwenda maeneo ya mbali na pia biashara zinazotoka viwasiwani kwenda visiwani ni pamoja na viwanyaji kama bia na bidhaa nyingine ambazo zinahitajika kwa binadamu,"amesema.

Ametaja baadhi ya visiwa ambavyo vitanufaika na kukamilika kwa miundombinu ya bandari ya Lushamba ni Kasarazi , Gembare, visiwa jirani vya kijiji cha Soswa, Namango, Chembaya, Chemagati na Zikagura .Pia kuna Kisiwa cha Maiosme ambacho nacho kipi kata jirani ya kata yao na kwamba kabla ya miundombinu kukamilika biashara hazikuwa nzuri kwani hakukua na muingiliano mkubwa watu lakini sasa biashara zimechangamka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...