Katibu
Tawala Mkoa wa Arusha ameipongeza wizara ya afya, maendeleo ya
jamii,jinsia, wazee na watoto kupitia idara ya maendeleo ya jamii kwa
kuona umuhimu wa kufanya mapitio ya sera yake ili kupata sera iliyo
shirikishi.
Ametoa
pongezi hizo alipokuwa akifungua kikao kazi cha mapitio ya sera ya
maendeleo ya jamii kwa kanda ya Kaskazini katika mkoa wa Arusha ambacho
kikao hicho kilijumuisha mikao ya Kilimanjaro, Tanga na Manyara.
“Ni
vizuri kufanya mapitio ya sera hii ili iweze kuendana na hali halisi ya
sasa hasa katika serikali hii ya viwanda katika uchumi wa kati kwa
kugusa makundi ya watu mbalimbali kama walivyo katika kikao hiki”.
Kwitega
amesema dunia imebadilika na mambo mengi yamebadilika hivyo hata pia
sera zetu zinapaswa kubadilika kulingana na mabadiliko haya hasa kwenye
maswala ya wanawake na watoto.
Hivyo
amewataka wadau wote walioshirikishwa kwenye kikao hicho kutoa maoni
yao ili kuwezesha kupata sera iliyobora na inayogusa takribani kila eneo
linalomgusa mwananchi wa hali yoyote.
Mkurugenzi
msaidizi wa idara ya maendeleo ya jamii Grace Magwa amesema, lengo
kubwa la kikao hicho ni kupitia sera ya maendeleo ya jamii ya mwaka 2000
ili ieleweke kwa wadau wakikao.
Amesema,
kisha wataitaji maoni kutoka kwa wadau hao katika kuboresha sasa sera
inayokuja na akasema ndio maana wamepita katika kanda zote 7
zinazojumuisha mikao yote 26 ya Tanzania bara ili kutoa nafasi kwa
wawakilisha wa makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika mchakato
huo.
Amesisitiza kuwa
maoni hayo yatakuwa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kuwa na sera
inayoendana na hali ya mabadiliko ya sasa ambayo yapo katika mabadiliko
ya hali ya mazingira, afya na maeneo mengine mengi hivyo sera nayo
inaenda kuzingatia mabadiliko hayo.
Bi
Mariam Mollel kutoka baraza la wafugaji Mkoa wa Manyara amesema, bado
kuna unyanyasaji mkubwa kwa wanawake katika kumiliki mali na kutoa
maamuzi katika jamii nyingi hasa za kimasai,hivyo kwa mapitio ya sera
hiyo itasaidia kuongeza vipengele vitakavyowezesha mwanamke kuepukana na
changamoto hiyo.
Kutokana
na mabadiliko mbalimbali katika jamii nyingi za Kitanzania, wizara ya
afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto imeamua kufanya zoezi
la kupitia na kukusanya maoni juu ya sera ya mwaka 2000 yenye mkakati
wake wa mwaka 2015 ambayo nayo ilirekebishwa kutoka katia sera ya mwaka
1992 ili kupata sera bora na shirikishi kwa miaka ijayo ambapo makundi
mbalimbali yalishirikishwa yakiwemo viongozi wa dini, watalaamu, taasisi
binafsi, na vyama mbalimbali vya kijamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...