Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakulima mara baada ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kubadili
matumizi ya gharama za uchimbaji wa visima kutoka Tsh Milioni 160 mpaka
kuchimba kwa Tsh Milioni 20.
Waziri
Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2019 wakati akizungumza na wananchi
mara baada ya kutembelea skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Mtwara.
Amesema
kuwa gharama za uchimbaji wa kisima kimoja kwa ajili ya umwagiliaji haipaswi
kuzidi shilingi Milioni 20 kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu na
kushindwa kuakisi kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Katika
ziara hiyo Waziri Hasunga ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuchimba visima
vitatu katika eneo hilo kwa kiasi cha shilingi milioni 60 ikiwa ni shilingi
milioni 20 kwa kila kisima kimoja.
Amesema
kuwa umefika wakati wa wakulima kuachana na kilimo cha kutegemea mvua za msimu badala
yake kuhakikisha kuwa wanalima kilimo bora cha umwagiliaji.
Kadhalika
amekumbushia agizo lake alilolitoa hivi karibuni la kila mkoa kuwa na Afisa
umwagiliaji wa mkoa huku wilaya zote zenye skimu za umwagiliaji kuwa na afisa
umwagiliaji wa wilaya.
Waziri
Hasunga amesema kuwa mkakati huo madhubuti wa serikali kuhakikisha kunakuwa na
skimu nyingi za umwagiliaji utaimarisha sekta ya kilimo jambo litakaloongeza
kipato cha mtu mmoja mmoja sambamba na Taifa kwa ujumla wake.
Kuhusu
mkakati wa serikali kuwa na kiasi kikubwa cha umwagiliaji, ameiagiza Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka miwili kuongeza eneo la
umwagiliaji ili kufikia hekta milioni moja huku kakiongeza kuwa hadi kufikia
mwaka 2025 eneo la umwagiliaji liwe limefikia Hekta milioni tano.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda amewapongeza wakulima wa
skimu hiyo kwa kuimarisha sekta ya kilimo huku akisisitiza kuwa serikali
inapaswa kuongeza mkakati madhubuti wa kuimarisha masoko ya mazao ya wakulima.
Kwa
upande wake Mkuu wa idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri Wilaya
ya Mtwara Ndg Joseph Tesha akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri wa Kilimo
amesema kuwa skimu hiyo ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere inayohudumia
vijiji vya Lilido na Chemchem ina jumla ya eneo la Hekta 920 zinazofaa kwa
kilimo cha umwagiliaji huku eneo lililoendelezwa likiwa ni jumla ya Hekta 310
pekee.
Waziri
Hasunga yupo mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo awali
alitembelea mkoa wa Pwani na Lindi kwa ajili ya kukagua hali ya
uuzaji wa korosho msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya
wakulima wa korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na
kukagua skimu za umwagiliaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...