Na Karama Kenyunko,Michuzi Globu
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ambapo a wasichana ameendelea kung'ara katika matokeo ya kidato cha nne na darasa la nne huku wavulana wakiongoza kwenye mitihani ya kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2019.
Katika matokeo yaliyotangazwa Leo Januari 9,2020 jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 10 bora tisa ni kutoka Shule ya Wasichana ya ST.Francis ya Mkoani Mbeya huku wengine wakitoka shule za Nyegezi na Sengerema Seminari za mkoani Mwanza, Feza Boy's (Dar es Salaam) na Shule ya Wasichana ya Huruma (Dodoma).
Dk Msonde amesema jumla ya watahiniwa wa shule 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wamefaulu katika mitihani wa kidato cha nne huki wasichana waliofaulu ni 175,296 sawa na asilimia 79.46 na wavulana ni 165,618 sawa na asilimia 81.94 na kwamba ubora wa ufaulu unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 135,301 sawa na asilimia 32.01 walipata daraja la kwanza hadi la tatu ambayo wasichana ni 58,542 sawa na asilimia 26.54 na wavulana ni 76,759 sawa na asilimia 37.97.
"Takwimu za matokeo zinaonesha watahiniwa wamefanya vizuri katika masomo mengi ya msingi ambayo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 51.25 na 91.31. Lakini hawakufanya vizuri katika masomo ya Fizikia na Hisabati licha ya ufaulu wa fizikia kuimarika kutoka asilimia 45.50 kwa mwaka 2018 hadi asilimia 48.38 2019," amesema Dk Msonde.
Akitaja Shule 10 bora Kitaifa katika mitihani wa kidato cha nne ni Kemebos (Kagera), Mtakatifu Francis (Mbeya), Feza Boy's na Canossa (Dar es Salaam), Shule ya Wasichana Anwarite (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha), Marian Boys' Mtakatifu Augustine Tagaste (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro na Musabe Boys (Mwanza).
Watahiniwa 10 bora Kitaifa ni Joan Ritte (Mtakatifu Francis), Denis Kinyange (Nyegezi Seminari), Erick Mutasingwa (Sengerema Seminari), Rosalia Mwidege (Mtakatifu Francis), Domina Wamara (Mtakatifu Francis), Mvano Cabangoh (Feza Boys') , Agatha Mlelwa, Sarah Kaduma na Shammah Kiunsi (wote Mtakatifu Francis) na Lucy Magashi (Huruma Girls).
Dk Msonde aliwataja wasichana 10 bora ni Joan Ritte, Rosalia Mwidege, Domina Wamara, Agatha Mlelwa, Sarah Kaduma, Shammah Kiunsi wote kutoka Shule ya Mtakatifu Francis, Lucy Magashi (Huruma Girls), Imani Sanga, Joyce Magwaza na Marther Ngowi (Mtakatifu Francis Mbeya).
Wavulana 10 bora Kitaifa ni Kinyange (Nyegezi Seminari), Mutasingwa (Sengerema Seminari), Cabangoh (Feza Boys'), Yohana Mwashambwa (Malangali- Iringa), Bruno Bruno (Don Bosco Seminari Iringa), Nelson Mbigili (St Dominic Savio-Iringa), Ebenezer Mujungu (Faraja Seminari ya Kilimanjaro), Timothy Mjuni, Richardson Kwareh na Henry Kimbori wote kutoka Centennial Seminari za Mkoa wa Pwani.
Pia alitaja Mikoa mitatu iliyofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne ambayo ni Kilimanjaro, Arusha na Iringa wakati hakuna mikoa iliyoshuka ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo.
Dk Msonde amesema halmashauri 10 zilizofanya vizuri katika mitihani huo ni Bagamoyo mkoani Pwani yenye shule 19, Bukoba mkoani Kagera, Meru mkoani Arusha, Mafinga mkoani Iringa, Kibaha mkoani Pwani, Njombe mkoani Njombe, Kibondo mkoani Kigoma, Kahama mkoani Shinyanga , Moshi mkoani Kilimanjaro na Bariadi mkoani Simiyu.
Ameaema halmashauri zilizoongeza ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo ni Madaba na Mbinga za mkoani Ruvuma, Mafinga (Iringa), Bukoba (Kagera) Mpimbwe (Katavi), Pangani (Tanga), Kasulu (Kigoma), Iringa (Iringa), Njombe (Njombe) na Kilolo (Iringa).
Aidha amezitaja halmashauri kumi zilizoshuka ufaulu kwa miaka 3 mfululizo kuwa ni, Mafia (Pwani), Kibiti (Pwani), Geita (Geita), Kakonko (Kigoma), Kondoa (Dodoma), Mpanda (Katavi), Kishapu ( Shinyanga), Kiteto (Manyara), Bumbuli (Tanga) na Malinyi (Morogoro).
"Takwimu za matokeo ya mitihani ya maarifa (QT) zinaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 7,070 sawa na asilimia 62,09 ya watahiniwa 11,386 wamefaulu mitihani hiyo. NECTA imefuta mitihani kwa watahiniwa 333 waliofanya udanganyifu katika mitihani ya kidato cha nne na kati ya watahiniwa waliofanya udanganyifu 142 wa mitihani ya darasa la nne, 29 wa kidato cha pili na 162 wa kidato cha nne," amefafanua Dk Msonde.
Ameongeza kuwa baraza hilo limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 538 ambao walipata matatizo ta kiafya na kushindwa kufanya upimaji wa masomo yote au mdai kubwa ya masomo na kwamba wanaruhusiwa kufanya mitihani hiyo kwa mwaka 2020 kwa mujibu wa kanuni za mitihani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Charles Msonde
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...