RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa hafla
ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wingwi
Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56
ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais ) Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na
(kushoto kwa Rais ) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.
Riziki Pembe Juma.(Picha na IKULU)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamede Shein, akimsikiliza Msimamizi
wa Mradi wa Jengo hilo Ndg. Peter Lazaro , wakati wa hafla ya Uwekaji wa
Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali Eng. Dkt. Idrisa Muslim Hija.(Picha na Ikulu)

WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Konde
wakiimba wimbo maalum wa kuwapongeza Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya
Sekondari ya Wingwi Wilaya ya Micheweni Pemba, ikiwa ni shamrashamra za
kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika
katika viwanja vya Skuli hiyo.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamede Shein akizungumza na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud
Mohammed, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya
Sekondari Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza Mtoto Fatma
Hamad Juma,Mwanafunzi wa Skuli ya Msingi Konde aliyeshiriki katika
kuimba wimbo Maalum na kutowa Salamu za Watoto wakati wa hafla ya
uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari Wingwi Mkoa wa Kaskazini
Pemba.(Picha na Ikulu)

WANANCHI wa Kijiji cha Wingwi
wakifuatilia hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya
Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea
Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika viwanja
vya Skuli hiyo.(Picha na IKULU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...