NA MWANDISHI WETU, MWANZA.
BODI ya Ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).
Katika ziara hiyo, Bodi hiyo imeweza kujionea utendaji kazi za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika maabara kubwa nacya kisasa iliyojengwa kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.
Aidha, bodi hiyo imeweza kufanya kikao chake cha kawaida, ikiwa ni cha kwanza kwa mwaka 2020.
Sambamba na hilo Bodi imekutana na watumishi wa TMDA kanda ya Ziwa ambapo Mwenyekiti wa MAB, Mhe. Balozi, Dkt. Ben Moses amewapongeza Menejimenti naxwatumishi kwa mafanikio ya utendaji kazi yaliyofikiwa na kuwahimiza kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuwezesha taasisi kufikia lengo lake la kuendelea kulinda afya ya wananchi kwa ufanisi zaidi.
Ziara ya wajumbe wa MAB inahusisha pia kutembelea na kujionea changamoto za udhibiti katika vituo vya Forodha vya Sirari na Mutukula.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMDA, Balozi, Dkt. Ben Moses (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB) yafanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya TMDA Kanda Ziwa, Mwanza ili kujionea utendaji kazi za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wadawa, vifaa tiba na vitendanishi. Ziara hiyo ambayo inahusisha pia vituo vya forodha vya Mutukula na Sirari imeenda sambamba na kikao cha kawaida cha Bodi kilichofanyika mapema Januari, 2020.

Mkurugenzi wa Huduma Za Maabara wa TMDA, Dkt. Danstan Hipolite akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya TMDA waliotembelea Maabara hiyo ya Kanda ya Ziwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...