Na Avila Kakingo, Michuzi Globu.

SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli imesema dhamira yake kubwa ni kuboresha mifumo  Bora ya Kielektroniki  ya ukusanyaji mapato na kuongeza uchumi kupitia mifumo ya Kielektroniki inayokidhi viwango vya kimataifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mipango wakati akifungua Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali Cha siku tatu pamoja na kuzindua mfumo mpya wa Uandaaji wa taarifa za fedha za majumuisho,Kikao hicho kimewakutanisha wahasibu kutoka taasisi zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali.

Waziri mpango amesema mfumo huo utapunguza gharama kwa Serikali pamoja na kuongeza usahihi wa taarifa kwa majumuisho ya Fedha za Serikali.

"Mifumo mingi madhubuti ya ukusanyaji mapato na matumizi ya serikali imeanzishwa ikiwa ni pamoja na mifimo uabuhasibu na rasilimali za umma zenye kukidhi biwango vya kimataifa. "

"Niseme tuu kwamba hii ndio Tanzania ambayo Rais Magufuli anatamanikuifikia yaani nchi yetu iwe ya kwanza katika kila jambotunalolifanya".

Aidha amewapongeza wataaalamu walioweza kutengeneza mfumo huo ambao utaokoa Fedha nyingi, huku akitoa rai kwa vijana na wataalam wa mifumo hiyo walioajiriwa  kuwajengea zaidi maadili ya kiwahasibu lengo ikiwa ni kuboresha mifumo mingine Bora zaidi,huku akitoa onyo kwa wahasibu wote watakaokiuka maadili kwa kujihusisha na Rushwa watachukuliwa hatua za kusheria .

Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Fransis Mwakapalila alibainisha majukumu ya Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali  ambayo ni kuandaa taarifa za Fedha za majumuisho za Serikali na kuziwasilisha kwa mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi Kama ilivyo matakwa ya sheria ya fedha hivyo mfumo huo utasaidia kwa kiasi kukubwa

Aidha amesema kuwa  hatua ya kuandaa Hesabu za majumuisho kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki unafanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutayarisha Hesabu za Majumuisho kwa kutumia mfumo ulioandaliwa na wataalam wake wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango

Awali akimkaribisha Waziri Mpango Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Marry Maganga alisema kuwa siku zote wamekuwa wakiwasisitiza wahasibu kufanya kazi kwa uzalendo, ubunifu na kuachana na kufanya Mambo kwa mazoea hivyo kikao kazi hicho kitaleta mabadiliko makubwa.

Hata hivyo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, amewapongeza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha na wote walioshiriki kufanikisha shughuli nzima ya mkutano huo.

Dkt Mpango ametoa rai kwa wahasibu wote nchini."Napenda nitoe rai kwenu kwamba, hakikisheni mafanikio haya tuliyoyapata yanakuwa endelevu. Pia, Hakikisheni kuwa usalama katika Mifumo yetu ya Fedha unakuwa madhubuti ili kuondoa uwezekano wa mifumo yetu kudukuliwa na kuleta hasara kubwa kwa Serikali na Wananchi".

Aidha amewakumbusha Wahasibu wote katika Utumishi wa umma kudumisha uadilifu na Uzalendo kwa nchi yetu.

Kikao kazi cha wahasibu wa Serikali kitadumu kwa muda wa siku tatu kikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uwezo wa kutumia mfumo mpya wa kuandaa Taarifa za fedha za Majumuisho za Serikali (Government Accounting Consolidation System - GACS) ambao umetengenezwa na watalaam wa ndani.

 Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt  Philip Mpango akizungumza wakati akifungua Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali Cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmmi,Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kufungua Kikao kazi  cha Wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Fransis Mwakapalila akizungumza mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Wageni waalikwa mbalimbali katika Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani)
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza,leo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...