Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), akiwa na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni CPA Aziz Kifile (Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali), Bw. John Sausi (Mkurugenzi wa Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa Fedha), CPA Francis Mwakapalila (Mhasibu Mkuu wa Serikali), Bi. Mary Maganga (Naibu Katibu Mkuu), CPA Pius Maneno Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), na CPA Evansi Asenga (Mkuu wa Hazina Ndogo Dar es Salaam)
Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius Maneno na Mkuu wa Hazina Ndogo Dar es Salaam CPA Evansi Asenga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Kuandaa taarifa za Hesabu za Majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa taarifa za Hesabu za Majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), wakifurahia jambo na Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Francis Mwakapalila (katikati) na Mkurugenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi, wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa taarifa za Hesabu za Majumuisho za Serikali kwa mwaka wa Fedha 2018/19, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wahasibu (CPAs) wanawake wakati wa ufunguzi wa kKikao Kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wahasibu wanawake (CPAs) wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa taarifa za Hesabu za Majumuisho za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).
Ramadhani Kissimba na Josephine Majura, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ameiagiza Menejimenti
ya Wizara ya Fedha na Mipango kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahasibu wote
wanaofanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya uhasibu kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi na rushwa.
Dkt. Mpango
alitoa maagizo hayo wakati akifungua Kikako Kazi cha kuandaa Hesabu za
Majumuisho za Serikali za mwaka 2018/19 pamoja na kuzindua Mfumo mpya wa
uandaaji wa taarifa za fedha za Majumuisho (Government Accounting Consolidation
System (GACS), Jijini Dar es Salaam
Dkt.
Mpango aliwataka wahasibu wote nchini kuwa wazalendo na kusimamia ipasavyo
matumizi ya rasimali za Umma na kuwataka kuhakikisha kuwa usalama
katika Mifumo ya Fedha unakuwa madhubuti ili kuondoa uwezekano wa mifumo hiyo kudukuliwa
na kuleta hasara kubwa kwa Serikali na Wananchi.
Aidha Dk. Mpango alimpongeza Mhasibu Mkuu wa
Serikali CPA Francis Mwakapalila, pamoja na Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha Bw.
John Sausi kwa kuonesha dhamira na nia ya kweli ya kuhakikisha wanatengeneza
Mifumo bora ya kifedha ili kuleta ufanisi mkubwa katika kukusanya na kuhasibu
mapato na matumizi ya Serikali.
Aliongeza
kuwa dhamira hiyo imedhihirika kwa
kuanzisha Mifumo ya Kifedha ya kimtandao kama Government e-payment Gateway
(GePG), Government Salary Payment Platform (GSPP), na sasa Government
Accounting Consolidation System (GACS).
‘’Nimefurahi
sana kuona kwamba ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne tangu Serikali ya
Awamu ya Tano iingie madarakani, mmeanzisha Mifumo mingi na madhubuti ya
kukusanya Mapato na Maduhuli ya Serikali, pamoja na Mifumo ya kuhasibu
rasilimali za umma yenye kukidhi viwango vya kimataifa” alisema Dkt. Mpango.
Aliongeza kuwa ni ushahidi bayana kuwa,
watendaji hao wanatafsiri kwa vitendo dhamira na dira ya Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Uongozi shupavu wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli ya kusimamia rasilimali
za nchi kwa manufaa ya Wananchi hasa
Wanyonge.
Pia alieleza kuwa matarajio ya Serikali ni kwamba mfumo huu
ulioanzishwa pamoja na Mifumo iliyokwisha kuanzishwa itaitumika vizuri kwa
weledi na uadilifu mkubwa katika kutoa huduma bora kwa Wananchi na ikizingatiwa
hilo matarajio ya wananchi na rasimali za umma zitatumika ipasavyo kuboresha
Maisha yao.
Awali
Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA. Fransis Mwakapalila alisema hatua ya kuandaa
Hesabu za Majumuisho kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki unaifanya Tanzania kuwa
nchi ya kwanza Barani Afrika kutayarisha Hesabu za Majumuisho kwa kutumia mfumo
uliandaliwa na wataalamu wake wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
CPA.
Mwakapalila alisema kwa sasa Tanzania ni nchi inayoongoza kwa ubora wa Taarifa
za FeFha za Majumuisho (CFS) zenye kukidhi viwango vya Kimataifa katika sekta
ya Umma (IPSAS) Barani Afrika.
Akizungumza
katika kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa fedha
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, amesema Idara yake itaendelea
kujenga mifumo ya kielektroniki ya fedha ili kuhakikisha makusanyo ya pesa za
Serikali yanapita katika mifumo sahihi.
“Mafanikio
yanayopatikana katika uandaaji wa mifumo hii yanatokana na watalaamu kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango kuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi yao, na
wataalamu hao wamekuwa wakiandaa mifumo mbalimbali ukiwemo mfumo wa kukusanya maduhuli ya Serikali kwa
njia ya Mtandao (GePG) ambapo Taasisi
zaidi 616 zimeshaunganishwa kwenye mfumo huo.
Bw.Sausi
alisema kuwa mfumo mpya wa uandaaji wa taarifa za fedha za majumuisho (GACS)
ambao umezinduliwa na Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango utasaidia kupunguza utiriri
wa kuwa na mifumo mingi ya uandaaji wa taarifa za fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...