

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitazama sampuli zilizopo katika Ofisi
ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu wakati
wa ziara yake kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika
picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu na Kanda ya Mbeya wakati wa ziara yake
kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Taasisi hiyo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………….
Na Mwandishi Wetu Tukuyu Mbeya
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameshuhudia
Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu
ilivyotelekezwa na kutojishughulisha na tafiti zozote ndaniya kipindi
cha muda mrefu.
Dkt. Ndugulile amebaini hayo
Tukuyu mkoani Mbeya wakati wa ziara yake katika Taasisi ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu kujionea utendaji wa Taasisi
hiyo.
Dkt. Ndugulile ameitaka Taasisi
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kurudisha Tawi la Tukuyu katika
hali yake ya awali kama ilivyokuwa ikisifika miaka ya nyuma ikiwa
imejikita katika taifiti.
Naibu Waziri Dkt. Ndugulile
ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kufanya tafiti
zaidi bila ya kutegemea sana wadau kwani zipo fedha za ndani
zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kufanya tafiti zikiwemo tafiti za
magonjwa ya binadamu.
Ameongeza kuwa kumekuwa na
matatizo mengi ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi ikiwemo kutumia
dawa bila kuwa na malaria, UTI na Typhoid ikiwa ni asilimia 70 ya homa
zikihusishwa na magonjwa hayo hivyo Taasisi hiyo ina nafasi kubwa ya
kufanya utafiti katika hili na kuwapa majibu wananchi.
“Nimesikitishwa sana na utendaji
kazi wa kituo hiki cha Tukuyu na wote naona mmehamia Mbeya nataka nione
mabadiliko katika Taasisi hiii hasa kituo hiki cha Tukuyu” alisema Dkt.
Ndugulile
Dkt. Ndugulile amemtaka
Mkurugenzi wa NIRM kusema kama hawana matumizi ya ofisi ya Tukuyu ili
itumike kwa matumizi mengine kwani haoni kinachofanyika katika Taasisi
hiyo nyeti katika tafiti za magonjwa ya binadamu nchini iliyopo Wilayani
Rungwe.
“Tunataka kukiona hiki kituo
kirudi katika heshima yake iliyokuwa nayo siku za nyuma hapa kusiwe ni
sehemu ya mapumziko ya watumishi bali kitumike kufanya tafiti”
alisema Dkt. Ndugulile
Kwa upande wake Mkurugenzi NIRM
Mbeya Dkt. Nyanda Elias Ntinginya amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa
bado wanahiitaji Ofisi ya NIRM Tukuyu kwani bado kuna tafiti
zinahitajika ili kuwasaidia wananchi.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo
itawakilisha mpango mkakati wa kuiendehsa Ofisi ya Tukuyu ndani ya mwezi
mmoja ili kuhakikisha Taasisi hiyoiatekelza majukumu yake ipasavyo
katika kuhakikisha inawasaidia kujibu maswali ya wananchi kuhusu
magonjwa ya binadamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...